HISTORIA YA ALIYEKUWA MMILIKI LEICESTER CITY VICHAI SRIVADDHANAPRABHA

Vichai Srivaddhanaprabha ni Mfanyabiashara na bilionea aliyezaliwa juni 5 mwaka 1958, miaka 60 iliyopita katika jiji la Bangkok nchini Thailand pia ndio C.E.O na Operetor wa kampuni ya King Power International Group ambayo inajishughulisha na maduka ya uuzaji wa vyakula kama SupperMarket na Shoppers.

Mnamo mwaka 2015 King Power ilizindua tovuti ya kuagizia vitu bure na nyingine ya kuagizia vitu kwa kulipia,baada ya kuanzishwa mwaka 1989.

Mnamo December 2009, kampuni ya King Power ilipokea kibali cha kifalme kutoka kwa mfalme wa Thailand katika sherehe ziliyohudhuria na Raksriaksorn, pia aliwahi kuorodheshwa na jarida la Forbes kuwa tajiri nambari 7 katika taifa hilo la Thailand akiwa na utajiri uliokadiriwa kufikia US dola Bilioni 3.3.

Agosti 2010, muungano wa uwekezaji wa soka wa barani Asia akiwa ni pamoja na Srivaddhanaprabha na mwanawe Aiyawatt walikubaliana kununuliwa kwa klabu ya Ligi ya Soka ya nchini Uingereza Leicester City, wakati huo ikicheza ligi ya Championships.

Suala hilo walifanikiwa na Milan Mandarić akiwa mwenyekiti wa klabu hiyo, mwezi February 2011 akiendelea kuwa mmiliki, na mtoto wake wa kiume Aiyawatt akawa kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo.

Mnamo July 2011, klabu hiyo ilibadili jina la kiwanja chake ambapo zamani kiliitwa jina la “Walkers Stadium” na badala yake kikaitwa King Power Stadium.
Baada ya uwekezaji huo wa bilionea huyo wa Kithailand klabu hiyo ilifanikiwa kufikia malengo ya tajiri huyo baada ya kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza EPL msimu 2015/2016, Muda mfupi kabla ya msimu huo wa 2015-2016, kumalizika Srivaddhanaprabha aliwazawadia wachezaji 19 magari aina ya BMW i8-£ 100,000 kila mmoja kama zawadi ya kushinda taji hilo.

Mbali na kuwa mmiliki wa Leicester City lakini pia mwaka 2017 aliinunua klabu ya Oud-Heverlee Leuven ambayo inashiriki ligi daraja B nchini Ubelgiji.

Lakini pia bilionea huyu ni mchezaji mzuri wa mchezo wa Polo mchezo unaochezwa kwa farasi na pia ni mmiliki wa klabu inayoshiriki mchezo huu ya VR Polo iliyopo nchini Thailand, lakini pia amewahi kuwa raisi wa klabu ya Ham Polo klabu iliyopo jijini London kuanzia mwaka 2008 hadi 2012.

Maisha yake binafsi Vichai Srivaddhanaprabha alizaliwa katika familia ya Kichina ya Thai Chinese alioana na Aimon Srivaddhanaprabha ambapo walibarikiwa kuwa na watoto wanne ambao ni Voramas, Apichet, Aroonroong na Aiyawatt.

Mwaka 2012 Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej alimpa jina la Srivaddhanaprabha likiwa na maana ya “Mwanaga endelevu wa utukufu” na mwaka 2016 alizawadiwa tuzo ya Doctor of Laws katika chuo cha Leicester.

Kwa imani yake kuwa mafanikio ya timu huathiriwa na Karma hivyo alikuwa anasafiri kwenda kuipatia dua timu hiyo kwa waumini wa Buddhist monks, kwa hiyo alijaribu kujenga hekalu la Buddhist na kuwasaidia watawa wa Buddhist kufanya karma kwa urahisi.na alikuwa na mahusiano ya karibu na Thai monk wanaojulikana kama Thai monk Phra Prommangkalachan ambaye mara nyingi walikuwa wakiwabariki wachezaji wa timu, ama ndani ya  Uingereza au katika hekalu la nyumba za watoni huko Thailand, Wat Traimit.

Na hawa Mabudda walikuwa wakisafiri kwenda kuikoa na kuisaidia timu ya Leicester na mwaka 2015 Aiyawatt aliweka kambi kwa Mabudda kama mwezi mzima.

Mnamo October 27, 2018 Vichai Srivaddhanaprabha akiwa kwenye Helcopter aina ya AgustaWestland AW169 ambayo ilikuwa imembeba tajiri huyo ilianguka nje ya uwanja huo na kulipuka,katika ajali hiyo walipoteza maisha watu watano akiwepo tajiri huyo wakati inaruka kutoka uwanjani.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema waliiona helcopter hiyo ikifanya mizunguka kadhaa juu kabla ya kushika moto na kudondoka na siku iliyofuata ilitolewa taarifa za kufa kwa bilionea huyo.

Kila mtu alisikitishwa na tukio hilo hasa wachezaji wa klabu ya Leicester City, huku siku ya jumatatu ya tarehe 29 ziliweza kutolewa heshima za mwisho kwa wadau, wachezaji pamoja na viongozi wa klabu hiyo katikati ya uwanja wa Leicester City.

Comments

Popular posts from this blog