Posts

Showing posts from September, 2016

TANGANZA BIASHARA YAKO KUPITIA BLOG YANGU

Image
Napatikana Bukoba mjini unaweza kutuma matangazo ya Biashara yako popote ulipo na na kutangazwa popote Tanzania kupitia blog yangu iyakayosambaza biashara kwenye magroup ya whatsaapp na Facebook n.k kwa bei rahisi kwa mawasiliano tumia namba 0756658100 au 0745874775

Tibaijuka ‘atema’ milioni 200/-

Image
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka amesema amekabidhiwa tuzo nchini Marekani, lakini amekataa kupokea fedha zinazoambatana na tuzo hiyo ambazo ni Dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200) kutokana na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo iliwahi kumtia matatani. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka alisema tuzo hiyo ni ya Maendeleo Endelevu ya Mwana wa Mfalme Khalifa bin Salman Al Khalifa wa Bahrain ambazo zilitolewa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani usiku wa Septemba 23, mwaka huu. “Tuzo hizi zinaambatana na fedha, lakini sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapa, niliwaambia naacha mezani nyie mtaamua cha kufanya maana kwa sheria ya nyumbani hatuna sheria ya kupokea zawadi,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye mwaka jana aliingia matatani baada ya kupewa Sh bilioni 167 zilizotokana na mgawo wa mfanyabiashara James Rugemarila kutokana na fedha za akaunti ya Tegeta Escrow katika...

Taarifa kuhusu kesi ya viongozi waliofungua akaunti bandia ya maafa Kagera

Image
Watumishi  watatu wa Serikali akiwamo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba wakituhumiwa kutaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu. Watumishi hao wanadaiwa kutaka kujipatia fedha hizo baada ya kufungua akaunti feki iitwayo kamati ya maafa Kagera kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu. Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo jana ni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantus Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, Mhasibu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB tawi la Bukoba, Carlo Sendwa. Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole, alidai watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili. Alilitaja shtaka la kwanza kuwa ni kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti iliyofunguliwa na Serikali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ...

Ajali ya boti ziwa Rukwa yaua watoto wawili

Image
Watoto  wawili wenye umri wa chini ya miaka miwili wamefariki dunia na watu wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria iliyokuwa imebeba abiria 29 kugonga kisiki na kuzama ndani ya ziwa Rukwa . Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema ajali hiyo imetokea wakati boti hiyo ikisafiri kutoka kisiwa cha uvuvi cha Kamsamba kwenda kambi ya uvuvi ya Nankanga wilayani Sumbawanga. Kamanda Kyando juhudi za kuwatafuta watu hao wawili zinaendelea na watu 25 waliokolewa wako katika hali nzuri kiafya baada ya kuokolewa na wasamalia wema waliofika eneo la tukio. Kamanda huyo wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni boti hiyo kugonga kisiki na kutoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini kwenye ziwa hilo kufuatana na wenyeji ambao wanajua sehemu za kupita kutokana na ziwa hilo kuwa na kina kifupi na visiki vingi. Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo ilipotokea ajali Mhe. Ignasi Malocha ameitaka ...

Msingi Imara Wa Mafanikio Yako

Image
Ipo faida kubwa maishani mwako endapo utaamua leo kuchukua hatua mathubuti ya kutaka kufanikiwa. Tupo hivi tulivyo kwa sababu hututaki kuchua hatua sitahiki za kiutendaji kwa yale yalipo akilini mwetu na kuyaweka katika matendo. Watu wana maarifa lakini suala la kuyaweka maarifa hayo katika matendo. Kuwepo kwa hali hii ndiyo ambayo inasababisha kuweza kuyatamani mafanikio na si kuyaishi. Hata hivyo moja ya siri nzito ya mafanikio yako husukumwa na kiu kubwa sana aliyonayo mtu  kutaka kufanikiwa, lakini kiu hiyohiyo huendana na msukumo na nia thabiti ya kuyaweka yale unayoyajua katika matendo. Nasisitiza hili kwa sababu moja kubwa watu wengi wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wameamua hali hiyo kutokea, lakini ili kuondokana na hali hii huna budi leo hii kuacha kuishi kikawaida kwa sababu wewe sio mtu wa kawaida. Huenda ukawa unajiona wewe ni mnyonge katika maisha kwa sababu labda uliwahi kufeli kwenye jambo fulani ambalo ulitegemea ya kwamba litakupa matokeo chanya lakini mat...

Simba Yaikalia Vibaya Yanga Suala La Kessy, Hatihati Kupoteza Pointi

Image
Simba imeikalia pabaya Yanga katika suala la beki Hassan Kessy na taarifa zinaeleza kwamba, iwe isiwe, huenda Yanga inaweza kupoteza pointi katika mechi zote ilizomtumia beki huyo. Taarifa zinaeleza, kamati iliyokuwa inalishughulikia suala hilo, imeona kuwa Kessy alikuwa bado ana mkataba na Simba wakati akisaini Yanga. “Kamati imeona hivyo, imewaambia Yanga na Simba wakutane na kulimaliza. Mkataba wa Kessy unatakiwa kuvunjwa kwa dola laki sita, Simba inaonekana wamepiga mahesabu yao, wamepunguza hadi aslimia kumi ambaye ni dola elfu sitini. “Hizi ni zaidi ya shilingi milioni mia ishiriki, si kidogo. Ndiyo maana kamati imesisitiza Simba na Yanga wakae wao na kumalizana. Sasa utaona hapa kuna shida. “Yanga lazima wawaangukie Simba, la sivyo mambo yatakuwa magumu kwao. Tena katika mechi alizocheza Kessy au kukaa benchi, kama kamati itapitisha ni batili au usajili wake una matatizo, pia watapokwa pointi. “Nafikiri aliyelishughulikia suala hili kama ni katibu wao...

Uingereza yatoa bil 6/- kusaidia waathirika wa tetemeko

Image
RAIS John Magufuli amepokea zaidi ya Sh bilioni sita kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ndege mbili za Serikali, Rais Magufuli alisema alikabidhiwa fedha hizo jana asubuhi na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke. Aidha, Rais Magufuli alisema wadau mbalimbali wametoa fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko hilo, lakini Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Amantius Msole pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda, waliamua kufungua akaunti inayofanana na iliyofunguliwa rasmi kwa ajili ya kukusanya fedha za msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko na kuanza kuzitafuna. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Katibu Tawala huyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba walikamatwa jana na kufikishwa mahakamani mjini Bukoba. Kutokana na maelezo ya Rais, baada ya Serikali kuchukua hatua hiyo iliyowapa imani wadau mbalimbali wanaojitolea kuc...

Viungo Simba, Yanga kuamua matokeo

Image
Mara nyingi ukifuatilia historia ya michezo ya mahasimu wa mji mmoja ‘Derby’ baina ya Simba na Yanga, matokeo ya mchezo huo mara nyingi huamuliwa na ufundi unaooneshwa eneo la kati la Uwanja Ubora wa wachezaji wanaocheza eneo hilo la uwanja, ‘Midfielders’ huweza kuamua matokeo kwa timu katika mchezo huo kutokana na aina ya washambuliaji waliopo katika timu zote mbili na mifumo wanayotumia. Mathalani, wachezaji kama Jonas Mkude, Mzamiru Yassini, Said Ndemla na Mohamed Ibrahim ndiyo unaofanya Simba kuonekana kuwa na utulivu na kuifanya timu hiyo imiliki mpira kwa muda mrefu huku ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga kutokana na viungo hao kupiga pasi nyingi kuelekea eneo la wapinzani. Inaweza kuwa tofauti kidogo kwa Yanga katika mfumo wa uchezaji kwa ujumla, hata hivyo ubora wa viungo si tofauti sana kutokana na Yanga kutokuwa na kawaida ya kumiliki mpira muda mrefu licha ya kuwa na viungo wazuri kama Haruna Niyonzima na Thaban Kamusoko. Niyonzima na Kamusoko w...

Hatukufungwa na Yanga mwaka jana, hawatufungi tena - Mashabiki Simba

Image
Wanachama wa klabu ya Simba wamesema wanaamini msimu uliopita hawakufungwa na Yanga na wanaamini wataibuka na ushindi katika mechi zote watakazokutana na watani wao. Mmoja wa wanachama wa klabu ya Simba ambaye pia ni mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa Ustaadh Masud amesema, msimu uliopita walicheza na Yanga wakashinda lakini kwa mazingira ya mchezo ulivyokuwa hawaamini kama walifungwa hivyo wanasubiria katika mchezo wa Jumamosi ili kuweza kubeba pointi tatu muhimu dhidi ya Yanga SC. Mgeni Ramadhani ambaye ni shabiki wa timu hiyo amesema, wameangalia mwenendo wa watani wao hivyo hawana sababu ya kushindwa kufunga lakini amewataka wachezaji wa Simba SC kutoidharau Yanga kwani mechi itakuwa ngumu tofauti na wanavyodhania. Kwa upande wake Telesphory Kiongozi ambaye ni Mwanachama wa Yanga amesema, wanaisubiri Simba SC na hawana sababu ya kuongea sana kwani wao ni watu wa vitendo zaidi hivyo wanasubiri dakika 90 za mchezo zimalizike ili waweze kuondoka na pointi tatu.

Ajali Ya Maajabu Jijini Dar

Image
Wapita njia wakitazama "maajabu" gari hili lililokuwa likitoka Mtongani kuelekea Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limeacha njia na kuparamia kingo ya barabara lakini lakustaajabisha wengi gari hilo liliparamia kingo hiyo kwa nyuma kama inavyoonekana.

Yaya Toure: Uamuzi wa Fifa utawaumiza wachezaji

Image
Yaya Toure alistaafu soka ya kimataifa wiki iliyopita Kiungo  wa Manchester City, Yaya Toure amesema wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka. Toure mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe katika kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia kutokomeza ubaguzi. Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura amesema kikosi kazi hicho kilikuwa na kazi maalumu ambayo tayari wameimaliza. Hata hivyo, hatua hiyo imekosolewa vikali na wadau mbalimbali, akiwemo Toure ambaye alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa CSKA Moscow Octoba mwaka 2013. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast amesema hatua hiyo ya FIFA itaweza kuwaumiza mashabiki na wachezaji kama mipango sahihi isipowekwa.

UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

Image
Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,    ==>Chuo Kikuu Ruaha     <<Bonyeza Hapa>>   ==> Chuo Kikuu Iringa     << Bonyeza Hapa>>   ==> Chuo kikuu Bugando   <<Bonyeza Hapa>>   ==>Chuo  Kikuu Cha Mwalimu Nyerere     <<bonyeza Hapa>>   ==>Chuo  Kikuu Cha  Udsm,duce Na Muce    <<bonyeza Hapa>>   ==>Chuo  Kikuu Cha  Tumaini Makumira     <<Bonyeza Hapa>>    ==>Chuo  Kikuu Cha Udom   <<bonyeza Hapa>>  ==>Chuo  Kikuu Cha Ifm  <<bonyeza Hapa>> ==>Chuo Kikuu Marian  << Bonyeza Hapa>>  ==>Chuo Kikuu Cbe         << Bonyeza Hapa>> ==>Tumaini-mbey...

Mo Dewji awatishia nyau Yanga ‘lazima wakae’

Image
Zikiwa  zimesalia siku chache kabla ya kupigwa kwa mechi ya wa watani wa jadi, Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya Oktoba mosi, tayari tambo za mashabiki zimeanza. Shabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ameandika ujumbe wa utani kwa mashabiki wa Yanga na kuwaambia kuwa siku hiyo watachezea kichapo. “Yanga lazima wakae, kandambili mahali pake ni uwani. #SimbaNguvuMoja,” aliandika MO. Hivi karibuni uongozi wa Simba ulikubali kufanya mabadiliko na kumruhusu Dewji kuwekeza kwenye klabu hiyo.

Tetemeko lang’oa vigogo 3 Kagera

Image
* Walifungua akaunti feki ya michango ya waathirika RAIS  Dk. John Magufuli, ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS), Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda, baada ya kubaini wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo “Kamati Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha. Uamuzi huo, umekuja siku 10 baada ya Rais Dk. Magufuli kuonya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa hayo kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha. Rais Magufuli alitoa kauli hiyo, Septemba 17, mwaka huu Ikulu, jijini Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya watu wote waliohusika katika...

Klopp: Liverpool wanaweza kutwaa taji Uingereza

Image
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema bado kuna nafasi ya kuimarika kama kikosi chake kinataka kupigania taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu hata baada ya kuanza vyema kampeni yao. Liverpool ambao mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa ligi ilikuwa mwaka 1990, waliicharaza Hull City kwa mabao 5-1 Jumamosi iliyopita na kupaa hadi mpaka nafasi nne katika msimamo, wakiwa nyuma ya vinara Manchester City kwa alama tano. Liverpool wameshinda mechi ngumu za ugenini dhidi ya Arsenal na Chelsea huku wakiwababua mabingwa Leicester City kwa mabao 4-1 msimu huu. Mechi pekee waliyopoteza ni ile waliyofungwa na Burnley. Akihojiwa, Klopp amesema ni kweli kwa sasa wanacheza vizuri lakini bado kuna nafasi ya kuimarika ili waweze kuendeleza wimbi lao la ushindi.

Gareth Southgate ndiye kocha wa muda wa England

Image
kocha msaidizi wa timu ya taifa ya England, ndiye anachukua nafasi ya kuinoa timu hiyo Southgate, anachukua nafasi hiyo baada ya Sam Allardyce kuachia ngazi kutokana na kashfa iliyomkumba. Allardyce maarufu kama Big Sam amedumu kwa siku 61 baada ya kupata mkataba mnono wa kuinoa England. Big Sam mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye mtego na kurekodiwa akipiga dili ya upindishaji wa sheria za FA. Southgate ataanza kuiongoza England katika mechi yake dhidi ya Malta Oktoba 8, ataingoza England kwa mechi nne kabla ya uamuzi wa suala la kocha mpya kutangazwa.

Lukas Podolski asikitishwa na maisha ya rafiki yake Schweinsteiger

Image
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Lukas Podolski, naye ameungana na wadau wa soka duniani wanaopinga maisha yanayomkabili kiungo Bastian Schweinsteiger kutoka nchini Ujerumani, chini ya kocha mpya wa Man Utd Jose Mourinho. Schweinsteiger amekua na maisha magumu tangu alipoanza msimu huu chini ya utawala wa Jose Mourinho na ilifikia wakati aliamrishwa kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa akiba, kwa kigezo cha kiwango chake kushindwa kumridhisha meneja huyo kutoka nchini Ureno. Podolski, ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, amesema hafurahishwi na mwenendo wa maisha ya rafiki yake huko Old Trafford ambapo kwa sasa pameonekana kuwa pachungu kwa Schweinsteiger . “Kama utafuatilia vizuri maisha ya Bastian, ninaweza kusema kwamba kinachotokea dhidi yake sio sahihi kwa mchezaji kama yeye ambaye ana heshima kubwa,” Podolski ameliambia jarida la Bild. “Sijui kwa nini Mourinho anamfanyia hivi, lakini ni wazi anachomtendea Bas...

Mtoto azaliwa kutoka kwa mbegu za watu 3

Image
Mtoto wa kwanza aliyetengezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa ,wanasayasi wamefichua. Mtoto huyo wa kiume mwenye miezi mitano ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake,babake pamoja na jeni za mfadhili. Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mamake kutoka Jordan anabeba katika jeni zake. Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyengine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida. Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika. Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini. Baadhi ya wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.

Tokea Ametua Ubelgiji, Takwimu Zinaonyesha Samatta Ni Hatari Zaidi Dakika 20 Za Mwisho

Image
Mshambuliaji Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk amefikisha mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubeligiji pamoja na mechi za Europa. Katika mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekan Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho. Kwani katika mabao hayo sita, ni bao moja tu dhidi ya Oostende katika mechi iliyochezwa Julai 31, ndiyo alifunga katika dakika ya 10. Lakini mabao mengine yote, amefunga kuanzia dakika ya 73 hadi 80, hali inayoonyesha kuwa kila dakika 20 za mwisho, ni mtu wa kuchungwa kweli. Mabao aliyofunga katika mechi za Europa ni dhidi ya NK Lokomotiva, alifunga katika dakika ya 83 na mechi ikaisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi ya pili dhidi ya timu hiyo, akafunga pia katika dakika ya 80.

EPL KESHO J/MOSI

BIG MATCH. EPL KESHO J,MOSI 24.SEP.2016 Manchester United  Kuwakaribisha mabingwa watetezi Leicester city Majira ya saa 8:00 Mchana, Huku ARSENAL akivaana na CHELSEA saa 1:30 jioni, Mechi zingine za mapema-  Manchester city wageni wa SWANSEA CITY, Liverpool vs Hull city, Bournemouth vs Everton, Middlesbrough vs Tottenham hotspurs, Stoke city vs West brom Sunderland vs C.palace. Mechi zote hizi majira ya saa 11:00 jioni. @SIKU NJEMA TUKUTANE KESHO TUONE NANI KUONDOKA NA PTS3.

HUU NDIO WIMBO MPYA WA EDWARD KISUSU -ATANIJIBU TU

http://soundofworshiptz.blogspot.com/2016/09/edward-kisusuatanijibu.html?m=0 Huu ndio wimbo mpya wa Muimbaji mahiri wa Nyimbo za Injili *Edward kisusu* uitwao .ATANIJIBU TU..uliofanywa na Producer SMART BILIONEA pale JB studio Akiongea na blogg Yetu amesema Yupo mbioni kutoa Video mpya ya ALBUM iitwayo UFUTE ALAMA Aliyomshirikisha CHRISTOPHER MWAHANGILA mzee wa Mungu ni Mungu tu ingia hapa kuidownload http://soundofworshiptz.blogspot.com/2016/09/edward-kisusuatanijibu.html?m=0  NISAIDIE KUSHARE UJUMBE HUU

HABARI NJEMA KWA WANAWAKE WOTE

HABARI NJEMA KWA WANAWAKE WOTE Hamna haja ya kwenda kwa waganga kumuwekea Mume wako Limbwata ili akupende zaidi au ili aende Kanisani. Inawezekana unatamani sana naye amwamini Mungu kama ilivyo kwangu, lakini bado hujafanikiwa kumbadili na anazidi kuwa mbaya zaidi. DAWA NI IPI? PETRO katoa dawa nzuri ya kumfanya Mume wako aamini Neno la Mungu, na kuenenda kama mtu mwenye hofu ya Mungu. Soma hapa; 1 Petro 3:1-6 [1] Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; [2] wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. [3] Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; [4] bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. [5] Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. [6] Kama vile Sara alivyomtii ...

Kauli ya Rais baada ya kupokea taarifa za vifo vya watu 13

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella kufuatia vifo vya watu 13 vilivyosababishwa na ajali ya barabarani iliyotokana na basi la abiria la Kampuni ya Super Shem kuligonga basi dogo la abiria (Daladala) katika kijiji cha Mwamaya kilichopo katika Kata ya Hungumalwa, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. Ajali hiyo imetokea  tarehe 21 Septemba, 2016 Majira ya saa 12:15 Asubuhi baada ya basi hilo dogo lililokuwa likitoka Kijiji cha Shirima kwenda Nyegezi Mjini Mwanza kuingia ghafla barabara kuu na kisha kugongwa na basi la Kampuni ya Super Shem lililokuwa likitoka Mkoani Mbeya kwenda Mwanza. Katika ajali hiyo watu wote 13 waliopoteza maisha na majeruhi 15 waliolazwa hospitali walikuwa abiria wa basi dogo lililogongwa. Rais Magufuli ameelezea kupokea taarifa za ajali hiyo kwa mshituko mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa imetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Watanzania wengine 12 wapoteze maisha katik...

Manchester united waondoa ukame wa magoal hapo jana baada ya kushinda 3-1

Image
Manchester United wamemaliza mkosi wao wa kupoteza mechi tatu mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa ugenini dhidi ya Northampton Town kwenye mchezo wa Kombe la EFL. Kocha wa Man United Jose Mourinho hakutaka kufanya makosa ambayo yangemgharimu na kusababisha kipigo kama alichopata kutoka kwa Manchester City, Watford na Feyenoord. Hata hivyo United itabidi wamshukuru sana kipa wa Northampton Adam Smith, ambaye makosa yake yalikuwa msaada mkubwa kwao katika mchezo huo baada ya kufanya makosa mawili makubwa yaliyopelekea kupatikana kwa magoli mawili ya United. Man United walipata mabao yao kupitia kwa Michael Carrick dakika ya 18, Ander Herrera dakika ya 68 na Marcus Rashford dakika ya 75. Northampton walipata goli lao pekee dakika ya 42 kupitia kwa Alexander Revell.

Mbinu bora ya kuishi maisha ya ushindi

Kwa mwanamichezo yeyote yule, anajua vyema ili aweze kushinda ni lazima atambue mbinu sahihi ya kumwezesha kushinda. Hivyo, kutokana na kujua hilo mara nyingi wanamichezo wengi huwa wanaweka mikakati na kutafuta mbinu bora kila siku za kuwawezesha kuwa washindi. Na mwisho wa siku kutokana na kutumia mbinu hizo ni kweli hujikuta ni washindi wa ndoto zao. Kama kwenye michezo iko hivyo, halikadhalika kwenye maisha ipo hivyo. Ili uweze kufanikiwa, inakulazimu ujue mbinu sahihi za kukuwezesha kufanikiwa. Wale wote wanaojua maisha pia yanahitaji mbinu, daima hufanikiwa na kuwa washindi. Moja ya mbinu bora ambayo wale waliofanikiwa huitumia sana kuweza kufanikisha ndoto zao ni kule kuishi kwa kufuata ndoto zao.  Hii ni mbinu bora sana ambayo hata wewe unahitaji kuitumia. Ikumbukwe mafanikio makubwa wakati wote yanaanza kwa kuishi kwa kufuata ndoto zako. Hutaweza kufikia ndoto zako hata kidogo, ikiwa utaishi maisha ya kutokufuata ndoto zako. Ni lazima ujue hasa ni kitu gani unachokitak...

Mourinho amgeukia Van gaal

Image
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anazidi kutafuta wa kumuangushia mzigo wa lawama kutokana timu hiyo kutofanya vizuri na kusema kwamba, wachezaji wake wanashindwa kufuata maelekezo yake kutokana na kuathiriwa na falsafa za kocha wao wa zamani Louis van Gaal. Manchester United wamepoteza mechi tatu mfululizo, na mchezo wa leo wa Kombe la EFL dhidi ya Northampton Town utakuwa muhimu katika kuhakikisha wanafuta hasira za mashabiki wao. Kwa takribani siku kumi Mourinho amekuwa akiwakosoa wachezaji wake hadharani, hali ambayo imekosolewa vikali na wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka, wakieleza kuwa masuala hayo yalitakiwa kumalizwa ndani kwa ndani. Mwezi uliopita bosi huyo wa United aliweka wazi kuwa, angekuwa na wakati mgumu sana kupandikiza falsafa zake kutokana na wachezaji wengi kuwa bado na falsafa za mtangulizi wake Van Gaal ambaye alidumu klabuni hapo kwa miaka miwili, akisema wachezaji hao walikuwa kama marobot. ‘Ni vigumu sana kubadilisha mfumo,’ alisema. ...

Baada ya Kilimanjaro Queens kubeba ubingwa jana

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani Kagera Bw. Salum Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake Kilimanjaro Queens kuwasili kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti wa Soka la wanawake Amina Karuma.Ongera Kilimanjaro Queens

Saida Karoli najihisi kuzaliwa upya

Image
#BURUDANI Saida Karoli afurahishwa na kitendo cha Diamond Platnumz kurudia kazi yake, asema kimemfanya ajihisi kuzaliwa upya maana hata waandishi wa habari sasa wameanza kumtafuta. Toa maoni yako. Soma:- http://www.eatv.tv/news/entertainment/najihisi-kuzaliwa-upya-saida-karoli

Hapa kasi tu

Image
Jiunge na kifurushi cha kimataifa upige simu Uingereza na sehemu nyingine mbalimbali kwa gharama nafuu Piga *149*71# . Tembelea hapa kufahamu zaidi http://bit.ly/2cxxK2K

Mfanye mwanamke kuwa kiumbe mwenye furaha

Image
MWANAMKE ● Anabadili Jina lake ● Anahama nyumbani kwao ● Anaacha familia yake ● Anaondoka na wewe ● Anajenga nyumba na wewe ● Anabeba ujauzito wako ● Ujauzito wako unabadili umbo lake ● Anakua mnene ● Anateseka chumba cha uzazi kwa maumivu makali kwa ajili ya mtoto wako. ● Na mtoto akizaliwa anasubiri umpe jina unalolipenda. Mpaka kifo chake atakufanyia kila kitu, kukupikia, Kusafisha nyumba yako, Kuwatunza wazazi wako, Kulea watoto, Kubana matumizi, Kukushauri, Kuhakikisha unapumzika, Kujenga mahusiano mazuri ya familia, Wakati mwingine anaweza hatarisha afya yake, Uhai wake kwa ajili yako. Anakufumania analia kisha anakusamehe. Mwanaume Muheshimu Mwanamke Katika Maisha yako, Sababu kuwa Mwanamke si jambo rahisi. Mfanye Mwanamke kuwa kiumbe mwenye furaha pindi unapokua nae maana Muda wa furaha kwake ni Mdogo sana. Shea kwa Heshima ya Wanawake wote Duniani. By Heri Lawama team.

Breaking news

Image
#Habari:Watu 12 wamefariki,na wengine 19 kujeruhiwa baada ya basi la New Force lililokuwa likitoka Dar kwenda Songea kupinduka baada ya kugongana na lori uso kwa uso huko kifanya mkoani Njombe usiku wa kuamkia leo.

Habari njema kwa wadau wa ligi ya Bundesliga

Image
Kwa mara nyengine tena, dawati lako la Spoti la DW linakuletea matangazo ya moja kwa moja ya ligi ya Ujerumani katika Deutsche Welle Bundesliga  Live, na mchuano wa Jumamosi hii ni kati ya Hamburger SV na FC Bayern München. Jiunge nasi saa 10.25 jioni  kwa  saa  za  Afrika Mashariki, ambapo mtangazaji wako mkongwe, Sekione Kitojo, akiwa na mchambuzi aliyebobea katika Bundesliga, Ramadhan Ali, pamoja na chipukizi Josephat Charo, wanakuletea mtanange huo moja kwa moja. Mshirikishe na mwenzio. WASHIRIKA WETU Unaweza  kusikiliza  matangazo  haya  kupitia  redio washirika wetu Afrika Mashariki  na Kati. Nchini Tanzania kupitia: Dar es Salaam: Capital FM, Mlimani FM, Wapo Radio Mkoani Kagera: Fadeco Community Radio na Kasibante FM Radio Tanga: Mwambao FM Mwanza: Radio Free Africa na Radio SAUT FM STEREO Mtwara: Pride FM na Safari FM Mbeya: Ushindi Radio Kenya washirika wetu ni: Nairobi: Radio Maisha Nyamira Kisii: Kisimaa...

Mpawa imekufikia

Image
Nafasi nyingine ya kuwapiga tafu washua ukiwa na #MPawa. Pata Mkopo wa hadi laki tano bila usumbufu wowote na jishindie milioni moja kila siku unapojiongeza na #MPawa kwa kuweka akiba kwenye kibubu chako. Bofya http://bit.ly/2chmqLI kufahamu zaidi.