Manchester united waondoa ukame wa magoal hapo jana baada ya kushinda 3-1

Manchester United wamemaliza mkosi wao wa kupoteza mechi tatu mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa ugenini dhidi ya Northampton Town kwenye mchezo wa Kombe la EFL.

Kocha wa Man United Jose Mourinho hakutaka kufanya makosa ambayo yangemgharimu na kusababisha kipigo kama alichopata kutoka kwa Manchester City, Watford na Feyenoord.

Hata hivyo United itabidi wamshukuru sana kipa wa Northampton Adam Smith, ambaye makosa yake yalikuwa msaada mkubwa kwao katika mchezo huo baada ya kufanya makosa mawili makubwa yaliyopelekea kupatikana kwa magoli mawili ya United.

Man United walipata mabao yao kupitia kwa Michael Carrick dakika ya 18, Ander Herrera dakika ya 68 na Marcus Rashford dakika ya 75.

Northampton walipata goli lao pekee dakika ya 42 kupitia kwa Alexander Revell.

Comments

Popular posts from this blog