Ajali ya boti ziwa Rukwa yaua watoto wawili

Watoto wawili wenye umri wa chini ya miaka miwili wamefariki dunia na watu wengine wawili hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria iliyokuwa imebeba abiria 29 kugonga kisiki na kuzama ndani ya ziwa Rukwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema ajali hiyo imetokea wakati boti hiyo ikisafiri kutoka kisiwa cha uvuvi cha Kamsamba kwenda kambi ya uvuvi ya Nankanga wilayani Sumbawanga.

Kamanda Kyando juhudi za kuwatafuta watu hao wawili zinaendelea na watu 25 waliokolewa wako katika hali nzuri kiafya baada ya kuokolewa na wasamalia wema waliofika eneo la tukio.

Kamanda huyo wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni boti hiyo kugonga kisiki na kutoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri wa majini kwenye ziwa hilo kufuatana na wenyeji ambao wanajua sehemu za kupita kutokana na ziwa hilo kuwa na kina kifupi na visiki vingi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo ilipotokea ajali Mhe. Ignasi Malocha ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kwenda katika ziwa hilo kuhakiki vyombo vya usafiri katika ziwa hilo ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

Comments

Popular posts from this blog