Mo Dewji awatishia nyau Yanga ‘lazima wakae’

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kupigwa kwa mechi ya wa watani wa jadi, Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya Oktoba mosi, tayari tambo za mashabiki zimeanza.

Shabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’ ameandika ujumbe wa utani kwa mashabiki wa Yanga na kuwaambia kuwa siku hiyo watachezea kichapo.

“Yanga lazima wakae, kandambili mahali pake ni uwani. #SimbaNguvuMoja,” aliandika MO.

Hivi karibuni uongozi wa Simba ulikubali kufanya mabadiliko na kumruhusu Dewji kuwekeza kwenye klabu hiyo.

Comments

Popular posts from this blog