Hatukufungwa na Yanga mwaka jana, hawatufungi tena - Mashabiki Simba

Wanachama wa klabu ya Simba wamesema wanaamini msimu uliopita hawakufungwa na Yanga na wanaamini wataibuka na ushindi katika mechi zote watakazokutana na watani wao.

Mmoja wa wanachama wa klabu ya Simba ambaye pia ni mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa Ustaadh Masud amesema, msimu uliopita walicheza na Yanga wakashinda lakini kwa mazingira ya mchezo ulivyokuwa hawaamini kama walifungwa hivyo wanasubiria katika mchezo wa Jumamosi ili kuweza kubeba pointi tatu muhimu dhidi ya Yanga SC.

Mgeni Ramadhani ambaye ni shabiki wa timu hiyo amesema, wameangalia mwenendo wa watani wao hivyo hawana sababu ya kushindwa kufunga lakini amewataka wachezaji wa Simba SC kutoidharau Yanga kwani mechi itakuwa ngumu tofauti na wanavyodhania.

Kwa upande wake Telesphory Kiongozi ambaye ni Mwanachama wa Yanga amesema, wanaisubiri Simba SC na hawana sababu ya kuongea sana kwani wao ni watu wa vitendo zaidi hivyo wanasubiri dakika 90 za mchezo zimalizike ili waweze kuondoka na pointi tatu.

Comments

Popular posts from this blog