HABARI NJEMA KWA WANAWAKE WOTE

HABARI NJEMA KWA WANAWAKE WOTE

Hamna haja ya kwenda kwa waganga kumuwekea Mume wako Limbwata ili akupende zaidi au ili aende Kanisani.
Inawezekana unatamani sana naye amwamini Mungu kama ilivyo kwangu, lakini bado hujafanikiwa kumbadili na anazidi kuwa mbaya zaidi. DAWA NI IPI?

PETRO katoa dawa nzuri ya kumfanya Mume wako aamini Neno la Mungu, na kuenenda kama mtu mwenye hofu ya Mungu. Soma hapa;

1 Petro 3:1-6
[1] Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;

[2] wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.

[3] Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;

[4] bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

[5] Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.

[6] Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.

Comments

Popular posts from this blog