Lukas Podolski asikitishwa na maisha ya rafiki yake Schweinsteiger

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Lukas Podolski, naye ameungana na wadau wa soka duniani wanaopinga maisha yanayomkabili kiungo Bastian Schweinsteiger kutoka nchini Ujerumani, chini ya kocha mpya wa Man Utd Jose Mourinho.

Schweinsteiger amekua na maisha magumu tangu alipoanza msimu huu chini ya utawala wa Jose Mourinho na ilifikia wakati aliamrishwa kufanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa akiba, kwa kigezo cha kiwango chake kushindwa kumridhisha meneja huyo kutoka nchini Ureno.

Podolski, ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, amesema hafurahishwi na mwenendo wa maisha ya rafiki yake huko Old Trafford ambapo kwa sasa pameonekana kuwa pachungu kwa Schweinsteiger .

“Kama utafuatilia vizuri maisha ya Bastian, ninaweza kusema kwamba kinachotokea dhidi yake sio sahihi kwa mchezaji kama yeye ambaye ana heshima kubwa,” Podolski ameliambia jarida la Bild.

“Sijui kwa nini Mourinho anamfanyia hivi, lakini ni wazi anachomtendea Bastian,sio sahihi.

“Meneja anapaswa kuwa muungwana na kujali utu wa mtu, lakini sio kwa Mourinho ambaye ameonyesha dharau kwa Schweini.”

Hata hivyo pamoja na Schweinsteiger kuungwa mkono na wadau wengi wa soka kwa kupinga anachofanyiwa na Jose Mourinho, bado ameonyesha hatua ya kutokua tayari kuihama Man Utd, jambo ambalo limepingwana Podolski .

“Nafikiri Marekani ni mahala sahihi kwake. Kwenda kucheza nje ya Ulaya kwa sasa ni sahihi kwa Schweinsteiger,”

“Ni wazi Schweinsteiger akienda Marekani atapata nafasi ya kucheza na heshima yake itarejea.” Aliongeza Podolski.

Comments

Popular posts from this blog