Gareth Southgate ndiye kocha wa muda wa England

kocha msaidizi wa timu ya taifa ya England, ndiye anachukua nafasi ya kuinoa timu hiyo

Southgate, anachukua nafasi hiyo baada ya Sam Allardyce kuachia ngazi kutokana na kashfa iliyomkumba.
Allardyce maarufu kama Big Sam amedumu kwa siku 61 baada ya kupata mkataba mnono wa kuinoa England.

Big Sam mwenye umri wa miaka 61, ameingia kwenye mtego na kurekodiwa akipiga dili ya upindishaji wa sheria za FA.

Southgate ataanza kuiongoza England katika mechi yake dhidi ya Malta Oktoba 8, ataingoza England kwa mechi nne kabla ya uamuzi wa suala la kocha mpya kutangazwa.

Comments

Popular posts from this blog