Simba Yaikalia Vibaya Yanga Suala La Kessy, Hatihati Kupoteza Pointi
Simba imeikalia pabaya Yanga katika suala la beki Hassan Kessy na taarifa zinaeleza kwamba, iwe isiwe, huenda Yanga inaweza kupoteza pointi katika mechi zote ilizomtumia beki huyo.
Taarifa zinaeleza, kamati iliyokuwa inalishughulikia suala hilo, imeona kuwa Kessy alikuwa bado ana mkataba na Simba wakati akisaini Yanga.
“Kamati imeona hivyo, imewaambia Yanga na Simba wakutane na kulimaliza. Mkataba wa Kessy unatakiwa kuvunjwa kwa dola laki sita, Simba inaonekana wamepiga mahesabu yao, wamepunguza hadi aslimia kumi ambaye ni dola elfu sitini.
“Hizi ni zaidi ya shilingi milioni mia ishiriki, si kidogo. Ndiyo maana kamati imesisitiza Simba na Yanga wakae wao na kumalizana. Sasa utaona hapa kuna shida.
“Yanga lazima wawaangukie Simba, la sivyo mambo yatakuwa magumu kwao. Tena katika mechi alizocheza Kessy au kukaa benchi, kama kamati itapitisha ni batili au usajili wake una matatizo, pia watapokwa pointi.
“Nafikiri aliyelishughulikia suala hili kama ni katibu wao, au kiongozi mwingine, hakuwa mzuri katika masuala ya mpira. Atakuwa ni mgeni au si mtu makini na ndiyo hivyo, Yanga sasa iko matatizoni katika hili,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Awali, Simba ilisema iko tayari kumuachia Kessy lakini Yanga ilitakiwa kuandika barua. Mwisho Yanga haikufanya hivyo, Simba ikaamua kulivalia njuga, hata hivyo baadaye TFF ilimpitisha kuichezea Yanga.
Comments
Post a Comment