Habari njema kwa wadau wa ligi ya Bundesliga
Kwa mara nyengine tena, dawati lako la Spoti la DW linakuletea matangazo ya moja kwa moja ya ligi ya Ujerumani katika Deutsche Welle Bundesliga Live, na mchuano wa Jumamosi hii ni kati ya Hamburger SV na FC Bayern München. Jiunge nasi saa 10.25 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ambapo mtangazaji wako mkongwe, Sekione Kitojo, akiwa na mchambuzi aliyebobea katika Bundesliga, Ramadhan Ali, pamoja na chipukizi Josephat Charo, wanakuletea mtanange huo moja kwa moja. Mshirikishe na mwenzio.
WASHIRIKA WETU
Unaweza kusikiliza matangazo haya kupitia redio washirika wetu Afrika Mashariki na Kati.
Nchini Tanzania kupitia:
Dar es Salaam: Capital FM, Mlimani FM, Wapo Radio
Mkoani Kagera: Fadeco Community Radio na Kasibante FM Radio
Tanga: Mwambao FM
Mwanza: Radio Free Africa na Radio SAUT FM STEREO
Mtwara: Pride FM na Safari FM
Mbeya: Ushindi Radio
Kenya washirika wetu ni:
Nairobi: Radio Maisha
Nyamira Kisii: Kisimaa FM
Webuye: Radio Mambo
Lamu: Sifa FM
Kitui: Wikwatyo FM
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo:
Bukavu: Radio Star
Kinshasa: Central FM
Uvira: Messenger du Peuple y Radio Ondese
Kalemi na Beni: Radio Francophones des Grands Lacs
Isiro: Radio Boboto Isiro
Bunia:RTK
Kisangani: Oped
Bukavu: Radio Universitaire ISDR
Beni: RTS
Uganda washirika wetu ni:
Tororo: Veros Radio
Mbale: Signal FM
Na pia kupitia satalaiti: SES-5 na Eutelsat 5W
Comments
Post a Comment