Mourinho amgeukia Van gaal

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anazidi kutafuta wa kumuangushia mzigo wa lawama kutokana timu hiyo kutofanya vizuri na kusema kwamba, wachezaji wake wanashindwa kufuata maelekezo yake kutokana na kuathiriwa na falsafa za kocha wao wa zamani Louis van Gaal.

Manchester United wamepoteza mechi tatu mfululizo, na mchezo wa leo wa Kombe la EFL dhidi ya Northampton Town utakuwa muhimu katika kuhakikisha wanafuta hasira za mashabiki wao.

Kwa takribani siku kumi Mourinho amekuwa akiwakosoa wachezaji wake hadharani, hali ambayo imekosolewa vikali na wadau na wachambuzi mbalimbali wa soka, wakieleza kuwa masuala hayo yalitakiwa kumalizwa ndani kwa ndani.

Mwezi uliopita bosi huyo wa United aliweka wazi kuwa, angekuwa na wakati mgumu sana kupandikiza falsafa zake kutokana na wachezaji wengi kuwa bado na falsafa za mtangulizi wake Van Gaal ambaye alidumu klabuni hapo kwa miaka miwili, akisema wachezaji hao walikuwa kama marobot.

‘Ni vigumu sana kubadilisha mfumo,’ alisema. ‘Ingekuwa rahisi zaidi kwangu kuwa na wachezaji wapya 20 na nianze mwanzo kila kitu.

‘Kwa miaka miwili walikuwa na wakitumia mfumo ambao ni tofauti na wangu.’

Ander Herrera ni moja ya wachezaji waliotolewa mfano kwamba wanachanganya namna ya uchezaji kati ya matumizi ya mfumo mpya wa Mourinho au ule wa awali wa Van Gaal.

Mabeki wa pembeni pia wanahangaika kuendana na mfumo mpya. Mourinho anawataka kupanda na kupeleka mashambulizi kwa kasi, wakati walikuwa wakielekezwa tofauti chini ya utawala wa Van Gaal.

Comments

Popular posts from this blog