TUNAFELI MAISHA BAADA YA SERENGETI BOYS.
NA GHARIB MZINGA DAR ES SALAAM Mwanzoni mwa mwaka 2019 Taifa letu linatarajia kupokea michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Timu za Chini ya umri wa miaka 17 (U17). Sina shaka kama taifa tunaisubiri kwa hamu michuano hiyo kwani tunaamini kwamba kikosi chetu kitafanya vema tukizingatia tupo nyumbani. Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu FIFA waliamua kuandaa michuano hiyo wakijua kila taifa linatakiwa kufanya maandalizi ya msingi katika uwekezaji wa mpira wa miguu. Sisi kama watanzania Timu zetu za vijana zimekua zikitupatia ile furaha tunayoikosa kwa miaka mingi kutoka timu ya wakubwa (Taifa stars). Vijana hawa kama tutawaendeleza vema naamini tutapata package kubwa ya Wachezaji wa kulisaidia taifa siku chache huko mbele. Tatizo kubwa ni kuwavusha kutoka hapo walipo mpaka kuipata stars. Hii ni changamoto kubwa ambayo inahitaji nguvu ya ziada ili kuhakikisha tunajenga taifa lenye uwezo. Taifa letu lina uhaba wa Mawakala, fursa hii imekua kiza kinene, wadau wengi hawaioni ...