KAKOLANYA KUTUA SIMBA DIRISHA HILI DOGO LA USAJILI

Imeelezwa kuwa golikipa nambari moja wa klabu ya Yanga Beno Kakolanya anatarajiwa kujiunga na klabu ya Simba katika dirisha hili dogo la Usajili.

Kakolanya anayedaiwa kugoma kutokana na kutolipwa mshahara wa miezi minne ndani ya klabu ya Yanga ndio atatumia kipengele hicho kuvunja mkataba na klabu ya Yanga ili apate nafasi ya kujiunga na klabu ya Simba SC.

Meneja wa mchezaji huyo Seleman Haroub ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba ndio amemushawishi nyota huyo kujiunga na Simba.

Taarifa hizo zinakuja baada ya kudaiwa kuwa klabu hiyo inahitaji golikipa mwenye uwezo sawa na Aishi Manula ili kumpa changamoto.

Aidha inaelezwa kuwa klabu ya Simba inajiandaa kuwatoa kwa mkopo magolikipa wake wawili ambao ni Emmanuel Mseja na Said Mohammed hivo itabakiwa na magolikipa watatu tu ambao ni Aishi Manula, Deogratius Munishi na Ally Salim.

Iwapo klabu hiyo itamsajili Beno Kakolanya atakuwa golikipa wa nne baada ya kuwatoa wale wawili kwa mkopo.

Comments

Popular posts from this blog