RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA WIKI HII

Ligi Kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 15, inatarajiwa kuendelea kwa michezo kadhaa kupigwa siku za Jumapili, Jumatatu na Jumanne.

Timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo zitashuka dimbani isipokuwa michezo inayozihusisha timu za Mtibwa Sugar na Simba zinazoshiriki michuano ya CAF.

HII HAPA NI RATIBA YA MICHEZO HIYO YOTE

Jumapili ya December 02-2018, itapigwa michezo minne katika viwanja tofauti tofauti.

Lipuli Fc wataikaribisha Biashara United ya Mara saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Mbeya City wao watawakaribisha African Lyon saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Kagera Sugar watawakaribisha Alliance Schools Fc ya Mwanza saa 10:00 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Na mchezo wa mwisho December 02, utakuwa kati ya Ndanda Fc dhidi ya Mbao Fc ya Mwanza saa 10:00 kwenye Uwanja wa Nangwanda, Mtwara.

Raundi ya 15 itaendelea Jumatatu ya December 03 kwa michezo mitatu itakayopigwa kwenye viwanja vitatu tofauti.

JKT Tanzania wataikaribisha Ruvu Shooting saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Meja General Isamuhyo.

Mwadui Fc wao watawakaribosha KMC ya Kinondoni saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Tanzania Prisons watawakaribisha Young Africans saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya.

Na mchezo wa mwisho wa raundi ya 15 utakuwa kati ya Azam Fc watakaoikaribisha Stand United saa 1:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex (Chamanzi), Jijini Dar es salaam.

Comments

Popular posts from this blog