ZANA AANZA MAZOEZI BAADA YA KUSAINI TU, JUUKO PIA YUPO
Baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba mapema leo, Zana Coulibaly ameanza mazoezi na kikosi cha Simba jioni ya leo.
Coulibaly amejumuika na wachezaji wengine wa Simba kwa mara ya kwanza kwenye mazoezi hayo yanayofanyika uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam.
Mlinzi huyo wa kulia ambaye pia anaweza kucheza nafasi ya ulinzi wa kati ya kiungo, amesajiliwa na Simba kuziba pengo la Shomari Kapombe anayetibiwa nchini Afrika Kusini baada ya kuvunjika mguua akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania.
Aidha katika mazoezi ya leo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani Jijini Dar es salaam, beki wa kati wa kimataifa Juuko Murshid ameyaudhulia kikamilifu.
Juuko amerejea na kujiunga na Simba baada ya kubakia kwao Kampala, Uganda ambako ilielezwa alibaki kwa ajili ya matatizo ya kifamilia baada ya majukumu ya timu ya taifa.

Comments
Post a Comment