TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA YA NOVEMBER 30-2018
Juventus wataanza kumuangazia kiungo wa kati Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, iwapo mchezaji wa Arsenal raia wa Wales Aaron Ramsey, 27, atakataa kujiunga na klabu hiyo ya Serie A. (Sun)
West Ham watampa nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City Samir Nasri mkataba mpya wa miezi sita iwapo atathibitisha kwamba yuko sawa kucheza. Mchezaji huyo mwenye miaka 31 amekuwa akifanya mazoezi na West Ham anapojiandaa kukamilisa marufuku ya kutumia dawa zisizoruhusiwa michezo, marufuku inayodumu hadi siku ya Mwaka Mpya. (Mirror)
Kinda wa Manchester City na Uhispania Brahim Diaz, 19, amefikia makubaliano yasito rasmi ya kujiunga na miamba wa Uhispania Real Madrid mwezi Januari. (Goal)
Mkurugenzi wa uchezaji wa zamani wa AC Milan Massimiliano Mirabelli anasema klabu hiyo ilijaribu kumnunua nyota wa Ureno anayechezea Juventus kwa sasa Cristiano Ronaldo, 33, majiraya joto yaliyopita, lakini wamiliki wa wakati huo wa AC Milan walipinga mpango huo. (Sportitalia kupitia Mail)
AC Milan wameanza mazungumzo ya kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Uhispania na Chelsea Cesc Fabregas, 31. (Calciomercato)
Manchester City wana nafasi nzuri sana ya kumnunua kinda wa Benfica kutoka Ureno mwenye miaka 17 Tiago Dantas. (Record, kupitia Manchester Evening News)
Mlinda lango wa Manchester United David de Gea, 28, anasubiri kuona iwapo Jose Mourinho atakuwa bado ndiye meneja wa klabu hiyo msimu ujao kabla ya kukubali kutia saini mkataba mpya katika klabu hiyo. (Mirror)
Arsenal na Tottenham wanaongoza katika mbio za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani anayechezea Hoffenheim Nadiem Amiri, licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye miaka 22 hajacheza mechi hata moja msimu huu kutokana na majeraha. (Bild kupitia Sun)
Watford wanamfuatilia kwa karibu winga wa England anayechezea Nottingham Forest Joe Lolley, 26. (Mail)
Meneja wa Burnley Sean Dyche amewatahadharisha mashabiki wa klabu hiyo wasitarajie 'mafuriko' ya wachezaji wapya kwenye klabu hiyo soko litakapokuwa wazi Januari licha ya kuteuliwa kwa Mike Rigg kuwa mkurugenzi wa kiufundi. (Lancashire Telegraph)
Meneja wa Aston Villa Dean Smith atafanya uamuzi kuhusu mchezaji James Collins ambaye amekuwa akifanyiwa majaribio katika klabu hiyo muda si mrefu. Beki huyo mwenye miaka 35 amekuwa bila klabu tangu kuihama West Ham majira ya joto na amekuwa akifanya mazoezi na Aston Villa. (Birmingham Mail)
Meneja wa Celtic Brendan Rodgers amesema beki wa Leicester Filip Benkovic, 21, ambaye yuko katika klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mmoja ni mchezaji stadi sana na kwamba yuko tayari kucheza Ligi ya Premia. (Daily Record, kupitia Leicester Mercury)
Arsenal wanatafakari uwezekano wa kuwafidia mashabiki takriban 800 waliokuwa wamenunua tiketi za kutazama mechi ya Europa League dhidi ya Vorskla ambayo ilihamishiwa Kiev kutokana na sababu za kiusalama Ukraine. (London Evening Standard)
Everton wamewasilisha ombi kwa baraza la mtaa wa Knowsley Council kutaka kujenga uwanja mpya wenye paa na kuhamisha uwanja wa wazi ambao umekuwepo katika eneo la mazoezi la klabu hiyo Finch Farm. (Liverpool Echo)
Kuna wanandoa Ufaransa ambao wanakabiliwa na mzozo wa kisheria baada ya kumbatiza mtoto wao Griezmann Mbappe, kwa heshima ya wachezaji wa Ufaransa walioshinda Kombe la Dunia Antoine Griezmann na Kylian Mbappe. Wanataka jina hilo likubalike kisheria, lakini hilo limepingwa na maafisa wa serikali. Maafisa waliopewa jukumu la kuidhinisha majina ya watoto wamekabidhi kisa hicho kwa waendesha mashtaka, na iwapo waendesha mashtaka hao watakubali kwamba jina hilo huenda likamsababishia mtoto huyo taabu baadaye maishani, mahakama ya masuaa ya kifamilia huenda ikaagiza familia hiyo kubadilisha jina la mtoto huyo. Mtoto huyo alizaliwa mapema mwezi huu mjini Brive katikati mwa Ufaransa (Sun)
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Sweden AIK wanauza 'kadi ya daima'ya kuhudhuria michezo uwanjani, bei yake ikiwa £16,000. Mwenye kadi hiyo ataendelea kuitumia hadi kifo 'kitakapomtenganisha na dunia'. Maajabu haya kwani huenda ukafa kesho, au ukabahatika kuishi miaka mia. (Independent)

Comments
Post a Comment