KILICHOMPONZA OKWI DHIDI YA MBABANE SWALLOWS

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema kuwa mshambuliaji nyota wa Simba Emmanuel Okwi alishindwa kuwa katika ubora wake kutokana na kufanya mazoezi muda mfupi na timu.

Okwi alishindwa kuonyesha makali katika mchezo wao wa kimataifa mbele ya Mbabane Swallows licha ya kusababisha penati iliyofungwa na mshambuliaji John Bocco.

"Okwi ni mchezaji mzuri, alishindwa kuonyesha uwezo wake kutokana na kutoka kuitumikia timu ya Taifa, alikosa mazoezi ya pamoja na timu ambayo ilibidi afanye kwa muda wa siku nne akafanya siku mbili, hivyo bado ana nafasi ya kufanya vizuri," alisema.

Mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane utachezwa Jumanne ya wiki ijayo ya December 4 kwenye uwanja wa Mavuso Sport Center uliopo jijini Mbabane nchini Eswatini zamani Swaziland.

Katika mchezo huo wa marejeano Simba wanatakiwa wasiruhusu kufungwa bao ili waweze kupita katika hatua hii.

Comments

Popular posts from this blog