SIMBA KUIFUATA MBABANE SWALLOWS SIKU HII
Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumapili ya December 02,2018 kuelekea Eswatini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumanne ya wiki ijayo ya November 04 kwenye Uwanja wa Mavuso Sport Centre uliopo jijini Mbabane nchini Eswatini zamani Swaziland.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema Simba inatondoka na msafara wa watu 30 utakaojumuisha wachezaji 21 na viongozi tisa wa benchi la ufundi.
Manara amesema Simba itaondoka Jumapili Alfajiri kwa usafiri wa shirika la Ndege la Afrika Kusini hadi nchini humo ambapo itatumia usafiri wa basi kwenda Eswatini.
Afisa Habari huyo amewaalika mashabiki wa klabu hiyo wanaotaka kusafiri na timu kuchangia kiasi cha dola 300 kwa safari ya kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini na dola 50 kwa safari ya kutoka Afrika Kusini hadi Eswatini.

Comments
Post a Comment