TUNAFELI MAISHA BAADA YA SERENGETI BOYS.
NA GHARIB MZINGA DAR ES SALAAM
Mwanzoni mwa mwaka 2019 Taifa letu linatarajia kupokea michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Timu za Chini ya umri wa miaka 17 (U17).
Sina shaka kama taifa tunaisubiri kwa hamu michuano hiyo kwani tunaamini kwamba kikosi chetu kitafanya vema tukizingatia tupo nyumbani.
Shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu FIFA waliamua kuandaa michuano hiyo wakijua kila taifa linatakiwa kufanya maandalizi ya msingi katika uwekezaji wa mpira wa miguu.
Sisi kama watanzania Timu zetu za vijana zimekua zikitupatia ile furaha tunayoikosa kwa miaka mingi kutoka timu ya wakubwa (Taifa stars). Vijana hawa kama tutawaendeleza vema naamini tutapata package kubwa ya Wachezaji wa kulisaidia taifa siku chache huko mbele.
Tatizo kubwa ni kuwavusha kutoka hapo walipo mpaka kuipata stars. Hii ni changamoto kubwa ambayo inahitaji nguvu ya ziada ili kuhakikisha tunajenga taifa lenye uwezo.
Taifa letu lina uhaba wa Mawakala, fursa hii imekua kiza kinene, wadau wengi hawaioni na wale wachache wanaojaribu hushindwa kufanya uwakala katika misingi yake.
Nimewagusa mawakala kutokana na nguvu yao kubwa ya kuwatafutia timu wateja wao. Baada ya Michuano ya vijana ya Afrika Mashariki kuwania kufuzu Afcon Mwakani nilitarajia kuona mawakala wakiwatoa hawa vijana kwa wingi.
Lakini wanaonekana kulala usingizi mzito, hao Mawakala wachache waliojaribu kuliendea jambo hili kwa Kelvin John 'Mbappe' na Morice Abraham hawaonekani kuwa na majibu ya kuridhisha.
Laiti kama mawakala wetu wangekua Active katika kuwatafutia Klabu na Vituo vya kukuzia vipaji huko ughaibuni, mwakani baada ya Afcon U17 wangekwenda katika vituo vyao kwaajili ya kujifunza zaidi, kwa njia hii kesho tungekua na idadi kubwa ya Wachezaji wenye ubora mkubwa kushindana popote.
Maisha ya vijana hawa kama tutaamua kuwaachia wenyewe waamue tutaendelea kuwa duni kila Leo Mwisho wake klabu za ligi kuu zitawabeba na kuwakandamiza huko chini na kubaki kaharibu karia yao kwa ujumla, Yupo wapi Nickson Kibabage na Yohana Nkomola ? Miongoni mwa majina yaliyotikisa sana kutoka kwenye Serengeti boys, Tusisubiri Papa aje awameze hawa vijana tena, tusawazishe makosa.
Naikumbuka ile Serengeti boys 2017 ya Bakari shime 'Gabon mpaka kombe la dunia' ambavyo ilikua na uwezo mkubwa mpaka kushiriki michuano ya Afrika ambapo iliweza kuwabana mbavu mabingwa mara mbili mfululizo Mali.
Baada ya ile michuano mawakala wa taifa la Mali hawakulaza damu kwa kuifanya kazi yao ipasavyo leo hii asilimia 75 ya vijana wa Mali wapo ulaya katika klabu kubwa, Abdoul Salam Ag Jiddou (AS Monaco) Mohammed Camara (Red Bull Salzbourg) Mamadou Samakè (Standard de Liège), Abdoulaye Diaby (Antwerp) Lassana N’Diaye (CSKA Moscou).
Wetu sisi wapo wapi ?
Hii inatafsiri kuwa hatuwezi kuwapa mazingira rafiki vijana wetu baada ya Maisha ya Serengeti boys.
Wakati wa michuano ya Kufuzu Afcon U17 ukanda wa Cecafa iliyofanyika Nchini mwaka huu, Kocha wa kikosi cha mabingwa Uganda Peter Onen alisema licha ya kutwaa taji lakini bado ana wachezaji 7 ambao hakuwa nao katika michuano hile kutokana na kwenda kufanya majaribio katika vituo na klabu mbalimbali ulaya.
Hii inaonesha kwa jinsi gani wenzetu walivyopiga hatua.
Licha ya January 2013 kushika nafasi ya 201 katika viwango vya ubora wa FIFA Taifa la Mauritania kwa Mara ya kwanza limefanikiwa kufuzu michuano ya Afcon 2019 Nchini Cameroon, lakini asilimia 40 ya Wachezaji wao ni matunda ya mawakala ambao waliowatoa vijana wa chini ya miaka 19 kwenda katika vituo vya mataifa mbali mbali barani ulaya ambao Leo ndio walioipeleka Mauritania pale Cameroon.
Miongoni mwa Wachezaji hao ni, Ally Abeid aliyetoka ASAC Concorde (Mauritania) kwenda levante Spain akiwa na miaka 17, -Bacary Moussa Ndiaye (17) Tevragh (Mauritania) kwenda Difaa el Jadida, -Moctar Sidi El Hacen (16) ASAC Concorde (Mauritania) kwenda Villadolid B Spain, - Mohamed Soudani (17), Kutoka Fc Nouadhibou (Mauritania) kwenda Stade tunisien, Abdillah Mahmoud (17) kwenda Deportivo Alaves Spain.
Shirikisho la soka Nchini (TFF) limefumba macho katika kuingia mikataba yenye kueleweka na mataifa na vituo mbalimbali vyenye uwezo wa kutusaidia, hizi ni hatua chanya kwa taifa lenye uvivu kama letu ikiwa ni plan ya Muda mfupi huku tukipigania plan ya muda mrefu. TFF na Mawakala waamke Watanzania wanataka furaha, "Why always us ?"

Comments
Post a Comment