CAMEROON YAPOKWA UENYEJI AFCON 2019.

Shirikisho la soka Afrika, CAF, limeipoka Cameroon uenyeji wa AFCON 2019 baada ya kutoridhishwa na maandalizi.

Katika mkutano mkuu unaoendelea jijini Acra Ghana, CAF imefikia uamuzi huo kufuatia ripoti mbili za uchunguzi kutoka kwa kamati ya usalama ya shirikisho hilo.

Ripoti ya kwanza ilikuwa na majibu ya ukaguzi uliofanywa kuanzia Otoba 27 Hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Ripoti ya pili ilikuwa na majibu ya ukaguzi uliofanywa kuanzia Novemba 11 Hadi Novemba 15.

Ripoti zote hizi zilionesha jinsi ambavyo Cameroon haikuwa tayari kwa kuandaa mashindano hayo makubwa barani humu.

Mwezi Oktoba, Rais wa CAF, Ahmad, alifanya ziara jijini Yaounde kukutana na  Rais wa Cameroon, Paul Biya, siku chache baada ya CAF ilipositisha mpango wa kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu nchi ya kuandaa mashindano hayo.

Kusuasua kwa Cameroon kuandaa AFCON 2019 kunatokana na ongezeko la timu kutoka 16 hadi 24, kitu kinachoongeza gharama za ujenzi wa miundombinu.

Kufuatia uamuzi huo, CAF itatoa mwezi mmoja kwa nchi zinazotaka kupatiwa haki ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2019, kuwasilisha maombi yao.

Morocco, ambao waliomba kuandaa Kombe la Dunia la 2026, wanapewa nafasi kubwa kuchukua  nafasi ya Cameroon. Waandaaji wa Kombe la Dunia 2010, Afrika Kusini, wanapigiwa chapuo pia.

Hii itakuwa mara ya pili katika siku za hivi kwa CAF kuipora nchi uenyeji wa  mashindano yake.

Septemba 2017, Kenya ilipokwa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN) na nafasi yake kupewa Morocco.

Mwaka 1995, Kenya hao hao, walipokwa nafasi ya kuandaa AFCON 1996 kutokana na sababu kama za Cameroon mwaka huu, Afrika Kusini wakachukua nafasi yake.

Comments

Popular posts from this blog