MWINGINE SINGIDA AVUNJA MKABATA SABABU NI ILE ILE

Mshambuliaji wa klabu ya Singida United, Tiber George, amevunja mkataba wake na klabu ya Singida United baada ya kushindwa kumlipa stahiki zake za kimkataba, imeelezwa.

Tiber alijiunga na Singida mwanzoni mwa msimu huu akitokea Ndanda FC ya Mtwara ambako alikuwa anakipiga na walima korosho hao kabla hajamaliza mkataba wake.

Inaelezwa kuwa, George kwa sasa sasa anatafuta timu ya kujiunga nayo kwenye dirisha hili la usajili ambalo limefunguliwa November 15 mwaka huu.

Nyota huyo ambaye alikuwa moja ya wachezaji tegemo klabuni hapo anasaka nafasi sehemu nyingine kabla ya dirisha la dogo la usajili kufungwa December 15.

Comments

Popular posts from this blog