Posts

Showing posts from January, 2018

USAJILI: BATSHUAYI ATUA DORTMUND KWA MKOPO

Image
Klabu ya Borussia Dortmund imekamilisha uhamisho mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu. Batshuayi ametua Dortmund ili kuziba pengo lililoachwa na Pierre-Emerick Aubameyang aliyesajiliwa na Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 56 na kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

BOFYA HAPA KUTAZAMA LIVE MECHI ZOTE ZA ULAYA LEO JUMATANO JANUARY 31-2018

Image
KUTAZAMA MECHI YA CHELSEA VS AFC BOURNEMOUTH BOFYA👉  HAPA  SAA 22:45 KUTAZAMA MECHI YA EVERTON VS LEICESTER CITY BOFYA ðŸ‘‰   HAPA  SAA 22:45 KUTAZAMA MECHI YA AC MILAN VS SS LAZIO BOFYA ðŸ‘‰  HAPA  SAA 22:45 KUTAZAMA MECHI YA TOTTENHAM HOTSPUR VS MANCHESTER UNITED BOFYA ðŸ‘‰   HAPA  SAA 23:00 KUTAZAMA MECHI YA MANCHESTER CITY VS WEST BROMWICH ALBION FC BOFYA ðŸ‘‰   HAPA  SAA 23:00 KUTAZAMA MECHI YA LEGANES VS SEVILLA BOFYA ðŸ‘‰  HAPA  SAA 23:30 USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

VIKOSI VINAVYOANZA VYA TOTTENHAM HOTSPUR VS MANCHESTER UNITED JANUARY 31-2018

Image
Lloris (C), Trippier, Sanchez, Vertonghen, Davies, Dier, Dembele, Eriksen, Dele, Son, Kane. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

USAJILI: RASMI OLIVER GIROUD ATUA CHELSEA

Image
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji Arsenal, Oliver Giroud kutoka kwa dau la Pauni Milioni 18. Arsenal imekubali kumuuza Giroud kwa mahasimu wao wa London baada ya kukamilisha usajili wa rekodi wa klabu yao wa Pauni Milioni 56 wa Pierre-Emerick Aubameyang. Dortmund ilikuwa tayari kumuuza Aubameyang mara tu itakampopata mbadala wake. Na tayari wameshampata mshambuliaji huyo wa Chelsea, Michy Batshuayi, baada ya  kufanyiwa vipimo vya afya nchini Ujerumani leo asubuhi. Baada ya usajili huo sasa Chelsea haitasajili mshambuliaji mwingine January hii, baada ya awali klabu hiyo kuwa katika mpango wa kuwasajili wachezaji kama Edin Dzeko wa Roma, Andy Carroll wa West Ham na hata mkongwe wa umri wa miaka 37 wa Stoke City, Peter Crouch. Oliver Giroud raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 ameitumikia Arsenal miaka mitano na nusu. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App...

HIKI HAPA KIKOSI BORA CHA HAJI MANARA MZUNGUKO WA KWANZA 2017-2018

Image
Afisa Habari wa klabu ya Simba Sc Haji Manara ametaja kikosi chake bora kwa mzunguko wa kwanza ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2017-2018. Manara ametaja kikosi hicho na kusema "hiki ni kikosi changu bora kwenye mzunguko wa kwanza wa VPL..nimezingatia mchango wa wachezaji binafsi kwa timu yake". HIKI NDICHO KIKOSI CHAKE BORA MZUNGUKO WA KWANZA MSIMU WA 2017-2018. Kikosi cha kwanza 1:Aishi Salum Manula-Simba Sc 2:Erasto Edward Nyoni-Simba Sc 3:Shafiq Batambuze-Singida United 4:Yakub Mohamed-Azam Fc 5:Asante Kwasi-Simba Sc 6:Papy Kabamba "Tshishimbi"- Young Africans 7:Shiza Ramadhan Kichuya-Simba Sc 8:Said Hamis Ndemla-Simba Sc 9:John Raphael Bocco-Simba Sc 10:Obrey Chora Chirwa-Young Africans 11:Emmanuel Anord Okwi-Simba Sc Kikosi cha Akiba 1:Razack Abalora- Azam Fc 2:Kelvin Yondan-Young Africans 3:Bruce Kangwa-Azam Fc 4:Mudathir Yahya-Singida United 5:Ibrahim Ajibu-Young Africans 6:Himid Mao-Azam Fc 7:Habib Kiyombo-Mbao Fc Mfumo 4-4-2...

USAJILI: RASMI PIERRE AUBAMEYANG ATUA ARSENAL KWA UAMISHO WA REKODI

Image
Kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger akipeana mikono Pierre-Emerick Aubameyang baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa Pauni Milioni 56. Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ya Ujerumani.    Aubameyang ametua Arsenal kwa uhamisho wa rekodi wa Pauni Milioni 56, na kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu. Klabu yake ya zamani ya Dortmund imethibitisha kupitia kwenye akaunti yake ya Twitter leo, kabla ya Arsenal kutoa picha za Aubameyang akiwa na jezi yao na akiwa na kocha Arsene Wenger.   Mchezaji huyo anaweka rekodi ya mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo Pauni 180,000 kwa wiki.  Kusajiliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutafungua milango ya mshambuliaji wa Arsenal, Mfaransa Olivier Giroud kuhamia Chelsea ambao nao watamruhusu Michy Batshuayi kwenda Dortmund kuziba pengo la Aubameyang kabla dirisha halijafungw...

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI (74 POSITIONS)

Image
Public service recruitment is looking for qualified candidates to fill the bellow Job Positions, the qualified candidates should apply by clicking the link on the Job Vacancy they are looking for:The bellow are the Job Vacancies needed to be filled BOFYA LINK HII HAPA USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

MICHEZO YA KIMATAIFA ITAKAVYO VURUGA RATIBA ZA SIMBA NA YANGA VPL

Image
Ligi Kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii ambapo vilabu vya Yanga na Simba vinavyoshiriki michuano ya Kimataifa vitashuka dimbani. Yanga itacheza Jumamosi, February 03 ikiwa ugenini mkoani Iringa dhidi ya Lipuli FC wakati Simba itakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na Ruvu Shooting. Baada ya mchezo huo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani February 06 kuivaa Njombe Mji kwenye uwanja wa Taifa huku Simba ikitarajiwa kupepetana na Azam FC February 07. Ikumbukwe Yanga itakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis February 10 huku Simba ikichuana na Gendermerie mchezo wa kombe la shirikisho February 11. Kuna taarifa kuwa uongozi wa Simba umeiandikia barua TFF kuiomba iahirishe mchezo wake dhidi ya Azam FC ili iweze kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho. Kama TFF itakubali maombi hayo ya Simba basi italazimika kuahirisha na mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji pia ili nayo ijiandae ipasavyo kuikab...

MALENGO YA EMMANUEL OKWI KUELEKEA KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Jumapili hii, kikosi cha Simba kitakuwa na wiki moja kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Gendarmeri ya Djibouti. Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa February 11, siku moja baada ya watani zao Yanga kuumana na St Louis kwenye michuano ya ligi ya mabingwa. Kinara wa mabao kikosi cha Simba Emanuel Okwi amesema wanapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo. Wasibweteke na mafanikio wanayopata kwenye ligi kuu ya Vodacom. Okwi amesema matokeo mazuri inayopata Simba katika Ligi Kuu sio kigezo cha timu hiyo kufanya vyema katika Kombe la Shirikisho. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda, anaongoza kwa kufunga mabao 12 katika Ligi Kuu yaliyochangia Simba kubaki kileleni kwa pointi 35. “Tunafurahi tumekuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi, sifa zinakwenda kwa timu nzima si mimi kufunga mabao na jambo la msingi ni kuongeza juhudi katika maa...

LICHA YA UFUNDI WAKE UWANJANI KAPOMBE AFUNGUKA HAYA KUHUSU AFYA YAKE

Image
Beki wa Simba, Shomary Kapombe amesema licha ya mashabiki kufurahia ufundi wake uwanjani, lakini anajiona bado hana ufiti wa asilimia mia wa kucheza kiwango anachokihitaji. Kapombe anasema anajijua jinsi anavyocheza akiwa fiti, jambo linalomfanya aongeze mazoezi ya ziada ili aweze kufanya kitu cha tofauti msimu huu. "Kiwango ninachokionyesha si cha Kapombe ninayejijua,bado nina safari ya kupambana ili niwe fiti zaidi, kikubwa ni mashabiki kuniombea ili nifikie lengo hilo litakalokuwa faida ya timu," alisema. "Nashukuru wachezaji wenzangu, walikuwa karibu na mimi , kipindi ambacho nilikuwa nje ya majukumu, ambapo niliweza kupitia mengi kama si kuyapuza nisingekuwa hapa,"aliongeza Kapombe. Anamtaja kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma kwamba alimsaidia kumjenga kisaikolojia na kumwambia atarejea kwa kasi kama ilivyo kwa sasa. "Djuma ni kocha wa aina yake, hapendi mchezaji ashindwe kufikia ndoto zake, alikuwa ananipa moyo wa kupambana na kuniambia maje...

SIMBA YAANZA KUIWINDA RUVU SHOOTING

Image
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre leo amekiongoza kikosi cha Simba kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting. Simba inajifua kwenye uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es salaam. Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa Jumapili ijayo kwenye dimba la Taifa. Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 7-0 dhidi ya timu hiyo kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza. Lechantre amesisitiza kuwa licha ya Simba kufunga mabao mengi, lakini hajaridhishwa na ukosaji wa mabao mengi pia. Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 35 kutoka michezo 15. Imefunga mabao 35 na kufungwa mabao sita pekee. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

KOCHA SIMBA ATAJA MECHI 3 ZA KUIPA UBINGWA

Image
Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba kufanikiwa kumaliza ikiwa kileleni, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Irambona Masoud Djuma, amesema bado hawajamaliza kazi ambayo wamepanga kuifanya msimu huu huku akitaja mechi tatu za kuwapa ubingwa. Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 35 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 30 wakati mabingwa watetezi Yanga wako katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 28 huku Singida United wenye alama 27 wakiwa nafasi ya nne. Djuma amebainisha kuwa kama Simba itapata ushindi katika mechi dhidi ya Yanga, Azam FC na Singida United, watakuwa wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa wa msimu huu. Djuma alisema kwa sasa hakuna timu yenye uhakika wa kuchukua ubingwa huo, lakini kumaliza wakiwa wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi tano kutoka klabu inayowafuatia ni jambo jema na litawafanya kupambana kuhakikisha wanaendelea kuwakimbia wapinzani wao. "Kikubwa tunamshukuru Mungu tumemali...

ASFC: TAZAMA MAGOLI NA PENATI ZOTE ZA IHEFU FC VS YOUNG AFRICANS JANUARY 30-2018

Image
TAZAMA HAPA MAGOLI YOTE YA IHEFU FC VS YOUNG AFRICANS JANUARY 30-2018 TAZAMA HAPA PENATI ZOTE IHEFU FC 3-4 YOUNG AFRICANS JANUARY 30-2018 USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

TETESI ZOTE ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO YA JANUARY 31-2018

Image
Roma inawasilisana na Manchester United kumhusu beki wa Uholanzi Daley Blind mwenye umri wa miaka 27. (Mirror) Viongozi wa ligi ya Serie A Napoli wameanzisha mazungumzo na Everton kwa azma ya kusaini mkataba na mchezaji wa kati Mholanzi Davy Klaassen, mwenye umri wa miaka 24, kwa mkopo hadi kufikia mwishoni mwa msimu. (Liverpool Echo) Meneja wa Newcastle Rafa Benitez amefanya mazungumzo ya dharura na mmiliki Mike Ashley na bado ana ''matumaini'' ya kusaini mkataba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji baadaye leo. (Mirror) Lakini Benitez anasisitizia msimamo wake ambao hautarajiwi kubadilika hata kama itashindikana kuhama kwa washambuliaji anaowalenga kama Islam Slimani na mlinzi wa Manchester City Eliaquim Mangala (Northern Echo) Arsenal itamruhusu mlinzi Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 32, kujiunga na Saint-Etienne kwa uhamisho wa bila malipo. (L'Equipe - in French) West Ham imezungumza na Lille kuhusiana na mpango wa kusaini mk...

SABABU YA SIMBA KUIANDIKIA BODI YA LIGI BARUA INAYOTAKA KUSOGEZWA MBELE MCHEZO WAO NA AZAM FC

Image
Klabu ya Simba ambao ni vinara wa ligi kuu Tanzania Bara hadi sasa ni kama wameanza kuingiwa na hofu baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kusogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam iliyopangwa kuchezwa February 07 mwaka huu. Simba yenye pointi 35, inachuana vikali na Azam wenye 30 katika msimamo wa ligi na Mabingwa watetezi Yanga waliovuna 28, katika kuliwania taji hilo la ubingwa wa ligi msimu wa 2017-2018. Afisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara alisema ratiba yao inawapa ugumu kutokana na akili na nguvu zao kuzielekeza kwenye michuano ya kimataifa na Simba imepangwa kucheza Gendarmerie Nationale ya Djibouti kati ya February 9-11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Manara alisema, ratiba hiyo inawapa ugumu kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting February 4 na kucheza na Azam kabla ya kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui Fx huku wakiusubiria mchezo wao wa kimataifa. “Mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na hiyo ndiyo sababu ya sisi kum...

RATIBA, MATOKEO NA MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA EPL

Image
👉 Matokeo ya jana Jumanne England - Premier League January 30 FT Swansea City 3 - 1 Arsenal FT West Ham United 1 - 1 Crystal Palace FT Huddersfield Town 0 - 3 Liverpool 👉 Ratiba ya leo Jumatano England - Premier League January 31 22:45 Chelsea vs AFC Bournemouth 22:45 Everton vs Leicester City 22:45 Newcastle United vs Burnley 22:45 Southampton vs Brighton & Hove Albion 23:00 Manchester City vs West Bromwich Albion 23:00 Stoke City vs Watford 23:00 Tottenham Hotspur vs Manchester United Huu ni msimamo wa ligi hiyo baada ya michezo mitatu ya jana Jumanne January 30-2018. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

RATIBA YA LEO NA MUDA KAMILI MECHI ZA AZAM SPORTS FEDERATION CUP (ASFC)

Image
Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), hatua ya 32 bora inatarajiwa kuendelea tena leo Jumatano ya January 31-2018 kwa mechi 7 zitakazopigwa katika viwanja tofauti. 👉 Ratiba kamili ya leo Jumatano ya January 31-2018 Azam Sports Federation Cup (ASFC). 14:00 Tanzania Prisons vs Burkina Fc 16:00 Majimaji Rangers vs Mtibwa Sugar 16:00 Njombe Mji vs Rhino Rangers 16:00 Pamba Sc vs Stand United 16:00 Kiluvya vs JKT Oljoro 16:00 Majimaji vs Ruvu Shooting 19:00 Green Warrios va Singida united USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

MAGAZETI YOTE YA MICHEZO TU YA LEO JUMATANO YA JANUARY 31-2018

Image
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

TANGAZO LA NAFASI MBALIMBALI ZA AJIRA HAPA NCHINI

Image
1:MEDICAL SPECIALIST II (RE ADVERTISED) – 1 POST Employer: Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) Date Published: 2018-01-29 Application Deadline: 2018-02-11 JOB SUMMARY: N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES: (xv)    Carry out ward rounds including teaching ward rounds; (xvi)    Attend emergency medical duties and responsibilities; (xvii)    Perform clinical duties and responsibilities in both private and public     outpatient clinics; (xviii)    Participate fully in morning clinical sessions, patients’ presentation and journal clubs; (xix)    Do researches in their respective medical fields; (xx)    Teach and supervise medical doctors, students and other health professionals in clinical works in his/her area of specialization; (xxi)    Participate in Medical Boards; (xxii)    Participate in outreach programs; (xxiii)    Participate in preparation ...

SAMATTA AREJEA GENK IKIPOTEZA UGENINI

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta alianza  kwenye kikosi cha kwanza cha KRC Genk ya Ubelgiji kilichocheza nusu fainali ya kwanza ya kombe la Beker van Belgie dhidi ya KV Kortrijk, mchezo uliofanyika usiku wa January 30-2018. Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza toka alipopata majera yaliyomfanya awe nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja. Samatta alipata majera ya goti November 4-2017, alipokuwa akiitumikia klabu yake na kushindwa kumaliza mchezo uliokuwa unapigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Luminus Arena. Samatta alifanyiwa uchunguzi kwa kina, na baada ya uchunguzi alilazimika kufanyiwa upasuaji na madaktari wakashauri akae nje kwa kipindi cha wiki sita hadi nane. Genk imepoteza mchezo huo ikiwa ugenini baada ya kufungwa goli 3-2, mchezo wa marudiano unatarajia kuchezwa February 6, 2018 kwenye uwanja wa nyumbani wa genk Luminus Arena. USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari ...

USAJILI BEKI WA ATHLETICO BILBAO ATUA MANCHESTER CITY

Image
Klabu ya Manchester City imefanikiwa kumsajiji beki wa Ufaransa Aymeric Laporte akitokea Athletico Bilbao kwa kitita kilichovunja rekodi ya timu hiyo cha £57M. Kitita hicho cha Laporte ambaye hajaichezea timu ya taifa ya Ufaransa , kinajumlisha gharama ya vilabu vya Uingereza mwezi huu kufikia £252m ikiwa ni rekodi katika uhamisho wa mwezi January. Kuwasili kwa mchezaji huyo ,mwenye umri wa miaka 23 kunajumlisha gharama ya klabu hiyo kuwanunua mabeki tangu mwisho wa msimu uliopita kufika £215.5M. Rekodi ya awali iliwekwa na kiungo wa kati wa klabu hiyo Kevin de Bryune aliyenunuliwa kwa kitita cha £55M 2015. ''Ninatazamia kufanya kazi chini ya mkufunzi Pep Guardiola na kujaribu kuisaidia klabu hiyo kupata ufanisi, aliumbia mtandao wa klabu hiyo. Inamaanisha kwamba klabu hii imeniamini na nafurahia kushirikiana nayo''. Wasiwasi kuhusu jeraha la beki Vincent Kompany mbali na wasiwasi mwengine kuhusu kutokuwepo kwa Eliaquim Mangala kumemshinikiza Guardiola ...

HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA QT 2017

Image
Baraza la Mitihani Tanzania –NECTA, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne na Maarifa –QT, ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ikilinganishwa na mwaka jana 2016. Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, alitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Jumla ya Watahiniwa laki 2 elfu 87 na 713 ambao sawa na asilimia 77.09% kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu, ambapo kati ya hao wasichana ni laki 1 elfu 43 na 728 sawa na asilimia 75.21%, wakati wavulana ni laki 1 elfu 43 na 985 sawa na asilimia 79.06%. Alifafanua kuwa Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa laki 2, elfu 77 na 283, ambao ni asilimia 70.09%, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 Mbali na hilo, Msonde ameweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo, ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30 mwaka 2017 mpaka Novemba 17, mwaka 2017. KUTAZAMA MATOKE...

HAYA HAPA MAGAZETI YOTE YA LEO JUMATANO YA JANUARY 31-2018

Image
UNAWEZA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017 KWA KUBOFYA  HAPA UNAWEZA KUTAZAMA MATOKEO YA QT 2017 KWA KUBOFYA  HAPA USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako