MALENGO YA EMMANUEL OKWI KUELEKEA KOMBE LA SHIRIKISHO
Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Jumapili hii, kikosi cha Simba kitakuwa na wiki moja kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Gendarmeri ya Djibouti.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa February 11, siku moja baada ya watani zao Yanga kuumana na St Louis kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.
Kinara wa mabao kikosi cha Simba Emanuel Okwi amesema wanapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Wasibweteke na mafanikio wanayopata kwenye ligi kuu ya Vodacom.
Okwi amesema matokeo mazuri inayopata Simba katika Ligi Kuu sio kigezo cha timu hiyo kufanya vyema katika Kombe la Shirikisho.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda, anaongoza kwa kufunga mabao 12 katika Ligi Kuu yaliyochangia Simba kubaki kileleni kwa pointi 35.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

“Tunafurahi tumekuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi, sifa zinakwenda kwa timu nzima si mimi kufunga mabao na jambo la msingi ni kuongeza juhudi katika maandalizi ya mashindano ya kimataifa,”alisema mshambuliaji huyo mwenye kiwango bora msimu huu.Okwi amesema kila mchezaji anatakiwa kuweka malengo ya kucheza kwa kiwango bora mashindano ya kimataifa mwaka huu.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako
Comments
Post a Comment