SABABU YA SIMBA KUIANDIKIA BODI YA LIGI BARUA INAYOTAKA KUSOGEZWA MBELE MCHEZO WAO NA AZAM FC

Klabu ya Simba ambao ni vinara wa ligi kuu Tanzania Bara hadi sasa ni kama wameanza kuingiwa na hofu baada ya kuitaka Bodi ya Ligi (TPLB) kusogeza mbele mechi yake dhidi ya Azam iliyopangwa kuchezwa February 07 mwaka huu.

Simba yenye pointi 35, inachuana vikali na Azam wenye 30 katika msimamo wa ligi na Mabingwa watetezi Yanga waliovuna 28, katika kuliwania taji hilo la ubingwa wa ligi msimu wa 2017-2018.

Afisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara alisema ratiba yao inawapa ugumu kutokana na akili na nguvu zao kuzielekeza kwenye michuano ya kimataifa na Simba imepangwa kucheza Gendarmerie Nationale ya Djibouti kati ya February 9-11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Manara alisema, ratiba hiyo inawapa ugumu kwani Simba itacheza na Ruvu Shooting February 4 na kucheza na Azam kabla ya kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui Fx huku wakiusubiria mchezo wao wa kimataifa.
“Mipango ya Simba ni kufika mbali katika michuano ya Afrika na hiyo ndiyo sababu ya sisi kumchukua kocha Mfaransa, Lechantre (Pierre) ambaye amewahi kuipa ubingwa wa Afcon, Cameroon mwaka 2000.
“Hivyo, basi kama uongozi tumeiomba Bodi ya Ligi kusogeza mbele mchezo wetu dhidi ya Azam ili kutupa nafasi ya kujiandaa na mechi yetu ya kimataifa dhidi ya Wadjibout kwa kuwa tunaona ratiba inabana sana.
“Tupo katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuiandikia bodi ya ligi ili kuwafahamisha mchezo huo usogezwe mbele na kikubwa tunataka kuona Simba ikifanya vema katia michuano hii ya mikubwa Afrika, tunaamini busura itatumika,”alisema Manara.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Comments

Popular posts from this blog