KOCHA SIMBA ATAJA MECHI 3 ZA KUIPA UBINGWA

Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara na Simba kufanikiwa kumaliza ikiwa kileleni, Kocha

Msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Irambona Masoud Djuma, amesema bado hawajamaliza kazi ambayo wamepanga kuifanya msimu huu huku akitaja mechi tatu za kuwapa ubingwa.

Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 35 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 30 wakati mabingwa watetezi Yanga wako katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 28 huku Singida United wenye alama 27 wakiwa nafasi ya nne.

Djuma amebainisha kuwa kama Simba itapata ushindi katika mechi dhidi ya Yanga, Azam FC na Singida United, watakuwa wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa wa msimu huu.

Djuma alisema kwa sasa hakuna timu yenye uhakika wa kuchukua ubingwa huo, lakini kumaliza wakiwa wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi tano kutoka klabu inayowafuatia ni jambo jema na litawafanya kupambana kuhakikisha wanaendelea kuwakimbia wapinzani wao.
"Kikubwa tunamshukuru Mungu tumemaliza mzunguko wa kwanza tunaongoza, lakini katika nafasi ya mbio za ubingwa naweza kusema tuna asilimia 55 mpaka pale tutakapocheza na wapinzani wetu, na tutaiona mapema kwa sababu mechi mbili kati ya Azam na Yanga tutacheza nao mapema na hapo tutaona mwelekezo," alisema Djuma.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Comments

Popular posts from this blog