SIMBA YAANZA KUIWINDA RUVU SHOOTING

Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre leo amekiongoza kikosi cha Simba kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting.

Simba inajifua kwenye uwanja wa Bandari, Tandika jijini Dar es salaam.

Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa Jumapili ijayo kwenye dimba la Taifa.

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 7-0 dhidi ya timu hiyo kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza.

Lechantre amesisitiza kuwa licha ya Simba kufunga mabao mengi, lakini hajaridhishwa na ukosaji wa mabao mengi pia.

Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 35 kutoka michezo 15. Imefunga mabao 35 na kufungwa mabao sita pekee.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Comments

Popular posts from this blog