USAJILI: RASMI OLIVER GIROUD ATUA CHELSEA
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji Arsenal, Oliver Giroud kutoka kwa dau la Pauni Milioni 18.
Arsenal imekubali kumuuza Giroud kwa mahasimu wao wa London baada ya kukamilisha usajili wa rekodi wa klabu yao wa Pauni Milioni 56 wa Pierre-Emerick Aubameyang.
Dortmund ilikuwa tayari kumuuza Aubameyang mara tu itakampopata mbadala wake.
Na tayari wameshampata mshambuliaji huyo wa Chelsea, Michy Batshuayi, baada ya kufanyiwa vipimo vya afya nchini Ujerumani leo asubuhi.
Baada ya usajili huo sasa Chelsea haitasajili mshambuliaji mwingine January hii, baada ya awali klabu hiyo kuwa katika mpango wa kuwasajili wachezaji kama Edin Dzeko wa Roma, Andy Carroll wa West Ham na hata mkongwe wa umri wa miaka 37 wa Stoke City, Peter Crouch.
Oliver Giroud raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 ameitumikia Arsenal miaka mitano na nusu.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako
Comments
Post a Comment