LICHA YA UFUNDI WAKE UWANJANI KAPOMBE AFUNGUKA HAYA KUHUSU AFYA YAKE
Beki wa Simba, Shomary Kapombe amesema licha ya mashabiki kufurahia ufundi wake uwanjani, lakini anajiona bado hana ufiti wa asilimia mia wa kucheza kiwango anachokihitaji.
Kapombe anasema anajijua jinsi anavyocheza akiwa fiti, jambo linalomfanya aongeze mazoezi ya ziada ili aweze kufanya kitu cha tofauti msimu huu.
Kapombe anasema anajijua jinsi anavyocheza akiwa fiti, jambo linalomfanya aongeze mazoezi ya ziada ili aweze kufanya kitu cha tofauti msimu huu.
"Kiwango ninachokionyesha si cha Kapombe ninayejijua,bado nina safari ya kupambana ili niwe fiti zaidi, kikubwa ni mashabiki kuniombea ili nifikie lengo hilo litakalokuwa faida ya timu," alisema.
"Nashukuru wachezaji wenzangu, walikuwa karibu na mimi , kipindi ambacho nilikuwa nje ya majukumu, ambapo niliweza kupitia mengi kama si kuyapuza nisingekuwa hapa,"aliongeza Kapombe.Anamtaja kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma kwamba alimsaidia kumjenga kisaikolojia na kumwambia atarejea kwa kasi kama ilivyo kwa sasa.
"Djuma ni kocha wa aina yake, hapendi mchezaji ashindwe kufikia ndoto zake, alikuwa ananipa moyo wa kupambana na kuniambia majeraha ni kitu cha kawaida badala yake alinitaka nizingatie mazoezi na kile ninachoambiwa na daktari,"alimaliza Kapombe.USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako
Comments
Post a Comment