USAJILI BEKI WA ATHLETICO BILBAO ATUA MANCHESTER CITY
Klabu ya Manchester City imefanikiwa kumsajiji beki wa Ufaransa Aymeric Laporte akitokea Athletico Bilbao kwa kitita kilichovunja rekodi ya timu hiyo cha £57M.
Kitita hicho cha Laporte ambaye hajaichezea timu ya taifa ya Ufaransa , kinajumlisha gharama ya vilabu vya Uingereza mwezi huu kufikia £252m ikiwa ni rekodi katika uhamisho wa mwezi January.
Kuwasili kwa mchezaji huyo ,mwenye umri wa miaka 23 kunajumlisha gharama ya klabu hiyo kuwanunua mabeki tangu mwisho wa msimu uliopita kufika £215.5M.
Rekodi ya awali iliwekwa na kiungo wa kati wa klabu hiyo Kevin de Bryune aliyenunuliwa kwa kitita cha £55M 2015.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

''Ninatazamia kufanya kazi chini ya mkufunzi Pep Guardiola na kujaribu kuisaidia klabu hiyo kupata ufanisi, aliumbia mtandao wa klabu hiyo. Inamaanisha kwamba klabu hii imeniamini na nafurahia kushirikiana nayo''.Wasiwasi kuhusu jeraha la beki Vincent Kompany mbali na wasiwasi mwengine kuhusu kutokuwepo kwa Eliaquim Mangala kumemshinikiza Guardiola kuamini anahitaji beki mwengine wa kati mbali na John Stones na Nicolas Otamendi.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako
Comments
Post a Comment