MICHEZO YA KIMATAIFA ITAKAVYO VURUGA RATIBA ZA SIMBA NA YANGA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom mzunguuko wa 16 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii ambapo vilabu vya Yanga na Simba vinavyoshiriki michuano ya Kimataifa vitashuka dimbani.
Yanga itacheza Jumamosi, February 03 ikiwa ugenini mkoani Iringa dhidi ya Lipuli FC wakati Simba itakuwa uwanja wa Taifa kumenyana na Ruvu Shooting.
Baada ya mchezo huo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Yanga inatarajiwa kushuka tena dimbani February 06 kuivaa Njombe Mji kwenye uwanja wa Taifa huku Simba ikitarajiwa kupepetana na Azam FC February 07.
Ikumbukwe Yanga itakuwa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis February 10 huku Simba ikichuana na Gendermerie mchezo wa kombe la shirikisho February 11.
Kuna taarifa kuwa uongozi wa Simba umeiandikia barua TFF kuiomba iahirishe mchezo wake dhidi ya Azam FC ili iweze kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho.
Kama TFF itakubali maombi hayo ya Simba basi italazimika kuahirisha na mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji pia ili nayo ijiandae ipasavyo kuikabili St Louis.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Comments
Post a Comment