SAMATTA AREJEA GENK IKIPOTEZA UGENINI

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta alianza  kwenye kikosi cha kwanza cha KRC Genk ya Ubelgiji kilichocheza nusu fainali ya kwanza ya kombe la Beker van Belgie dhidi ya KV Kortrijk, mchezo uliofanyika usiku wa January 30-2018.

Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza toka alipopata majera yaliyomfanya awe nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Samatta alipata majera ya goti November 4-2017, alipokuwa akiitumikia klabu yake na kushindwa kumaliza mchezo uliokuwa unapigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Luminus Arena.

Samatta alifanyiwa uchunguzi kwa kina, na baada ya uchunguzi alilazimika kufanyiwa upasuaji na madaktari wakashauri akae nje kwa kipindi cha wiki sita hadi nane.

Genk imepoteza mchezo huo ikiwa ugenini baada ya kufungwa goli 3-2, mchezo wa marudiano unatarajia kuchezwa February 6, 2018 kwenye uwanja wa nyumbani wa genk Luminus Arena.
USISAHAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO, BOFYA LIKE Nijuzehabari Blog Ipo Play Store Pakua App Yetu Iliyoboreshwa HAPA Upate Habari Zote Mpya Moja Kwa Moja Kupitia Simu Yako

Comments

Popular posts from this blog