MAAMUZI YA YANGA KUHUSU KOMBE LA MAPINDUZI
Uongozi wa mlabu ya Yanga SC ya umesema kuwa hautapeleka kikosi kamili kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, ili kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jjini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwamba wanalazimika kuwapumzisha baadhi ya wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). Zahera amesema kwamba, Yanga kama klabu inatakiwa kuweka malengo kwenye vitu vyenye manufaa kwake, kwani wakiamua kutaka mataji yote wanaweza kujikuta wanakosa yote. “Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na Ligi Kuu, tupo na Azam Federation Cup, Mapinduzi Cup na Sport Pesa, inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu, tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kukosa yote, hivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwa ajili ya Li...