IDDI PAZI 'FATHER' ALIVYOCHAMBUA SAFU YA ULINZI YA SIMBA SC (CAF CL)
Ni sehemu ya pili ya mazungumzo ya Azam Tv na golikipa wa zamani wa klabu ya Simba, Idd Pazi ‘Father’ katika kipindi cha Sports AM, ambapo safari hii ameichambua timu ya Simba ambayo imefuzu kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL).
Mbali na hilo, Pazi amekumbushia mambo mengi mengi yanayohusu historia ya soka lake na klabu ya Simba miaka hiyo, hadi kipindi alichoaminiwa na kocha wake kuwa mpigaji wa penati licha ya kuwa golikipa.
Kama kawaida kipindi hiki baada ya mahojiano, Bin Zubeiry anaungana na wachambuzi Anuary Mkama, Yahya Kingoma na Jemedari Said kujadili matukio makubwa ya kimichezo yaliyojiri wikiendi hii kubwa ikiwa ni ushindi mfululizo wa Yanga na Simba katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Install Application ya Nijuze Habari Uweze Kupata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Comments
Post a Comment