MAYWEATHER AMPIGA 'KNOCKOUT' MARA TATU TENSHIN NASUKAWA

Floyd Mayweather alihitaji sekunde 140 pekee kumshinda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa katika pigano la maonyesho lililokuwa na thamani ya dola $9m.

Bingwa huyo mara tano wa zamani Mayweather mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo la muda mfupi mjini Tokyo alipombwaga mara tatu mpinzani wake mwenye umri wa miaka 20.



Pigano hilo la raundi tatu lilimalizika huku Nasukawa akibubujikwa na machozi baada ya kikosi chake kurusha kitambaa cheupe ndani ya ulingo kikitaka pigano kusitishwa.

Licha ya kurudi katika pigano hilo Mayweather alisema yeye amestaafu ndondi za kulipwa.

''Ni hatua ya kuburudisha tu, tulifurahia sana , alisema raia huyo wa Marekani ambaye alimshinda bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano la masumbwi mnamo mwezi Agosti 2017.

''Walitaka pigano hili kufanyika nchini Japan hivyobasi nikasema kwa nini lisifanyike?''

Pigano hilo lilicheleweshwa kwa saa kadhaa huku kukiwa na uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba huenda Mayweather asishiriki katika pigano hilo na kwamba waandalizi walikuwa wakishindwa kujua aliko.

Na baadaye alionekana akikuza klabu yake ya Las Vegas akiwataka watu kwenda kuona pigano hilo katika mgahawa huo.

Mabondia wote wawili walikuwa hawajashindwa kabla ya pigano hilo lililokosolewa ambapo Mayweather alikua na uzani wa juu wa kilo 4 dhidi ya mpinzani wake.

Baada ya kumshinda Nasukawa, Mayweather alisisitiza kuwa: Bado hajashindwa , Tenshin ni bondia mzuri sana.

Akimshauri bondia huyo alimtaka kutovunjika moyo na kuendelea.

''Nawataka mashabiki wote duniani kumuunga mkono Tenshin , ni mtu mzuri na bingwa''.

Sheria zilikuwa na masharti makali huku Nasukawa ambaye ni Kickboxer akionywa kupigwa faini ya dola milioni 5 iwapo atampiga teke mpinzani wake.

Hakukuwa na majaji huku Knockout ikiwa ndio ushindi. kabla ya pigano hilo bingwa wa zamani katika uzani wa Super Lightweight Amir Khan alisema kuwa pigano hilo ni ''mzaha mkubwa''.

Install Application ya Nijuze Habari Uweze Kupata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi

=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Comments

Popular posts from this blog