WAZIRI KALEMANI AWAWEKA KATI WAKANDARASI MIRADI YA UMEME

Waziri wa Nishati,  Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake.

Alitoa maagizo hayo wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ofisini kwa Mkuu wa Wilaya, Colonel Magembe, Waziri Kalemani alifafanua kwamba viongozi na wawakilishi wa wananchi ndiyo wanawajibika kuisemea serikali, hivyo wanapaswa kuifahamu kwa kina miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, waweze kuwaeleza wananchi.

“Hili ni agizo kwa wakandarasi wote wa miradi hii nchi nzima, wapatieni viongozi wa maeneo mnayofanya kazi mipango-kazi yenu, wajue nini mnatekeleza, kwa namna gani na kwa kipindi gani ili nao wasaidie kuwaelimisha wananchi wao,” alisisitiza Waziri.

Aidha, alitaja umuhimu mwingine wa viongozi kuelewa mipango-kazi ya wakandarasi kuwa itawawezesha kusimamia ipasavyo utekelezaji wake ikiwemo kuhoji pale ambapo watabaini mkandarasi anasuasua.

Waziri Kalemani anaendelea na ziara yake ya kazi aliyoianza Desemba 20, mwaka huu kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika mikoa mbalimbali ambapo anatarajia kuhitimisha Januari 2, mwakani.

Install Application ya Nijuze Habari Uweze Kupata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi

=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Comments

Popular posts from this blog