STEMPU ZA KIELEKTRONIKI ZA USHURU WA BIDHAA KUTUMIKA MWAKANI

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa
Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019.

Zitaanza kutumika rasmi katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa lengo la kuweka stempu za kielektroniki kwenye bidhaa hizo ni kupata idadi halisi ya uzalishaji wa bidhaa ili kutoza kodi stahiki na kuondoa dhana ya kusema kwamba TRA inawaonea wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa hizo kwa kutoza kodi isiyoendana na uzalishaji.

“Lengo la kuweka stempu hizi za kielektroniki ni kupata kiasi halisi cha uzalishaji wa bidhaa hizi ili kila upande uridhike yaani mzalishaji alipe kodi sahihi na sisi TRA tutoze kodi stahiki bila kupingana wala kugombana na wateja wetu”, alisema Kichere.

Install Application ya Nijuze Habari Uweze Kupata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi

=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Comments

Popular posts from this blog