Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini : Android ===> Google Play KIKOSI cha Zanzibar Heroes, kimeondoka Unguja leo kwenda Kenya kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yanayotarajia kuanza December 3 mwaka huu wakitumia usafiri wa basi na boti. Msafara huo wa watu 34, wachezaji 24 na viongozi 10, wamendoka majira ya saa 9:00 asubuhi na boti ya Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam, walipofika Dar es Salaam, walipanda basi kwenda Kenya, kwa kutumia njia ya Tanga. “Tumaini la safari yetu hii itakuwa yenye mafanikio makubwa kwa Zanzibar nzima, kikubwa tunaomba dua zenu tusafiri salama kwenda na kurudi,” alisema Kocha wa timu hiyo Hemed Suleiman ‘Morocco’. Miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Ahmed Ali ‘Salula’, NassorMrisho, Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’,Abdallah Haji ‘Ninja’, Mohd Othman Mmanga, Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ , Adeyum Saleh ‘Machupa’, Haji Mwinyi...