BEKI MTIBWA SUGAR ASAINI MKATABA MPYA

Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:

Klabu ya Mtibwa Sugar imemsainisha mkataba wa miaka miwili beki wake wa pembeni  Nickson Kibabage ili  kuendelea kuitumikia  klabu ya Mtibwa Sugar yanye makazi yake mkoani Morogoro.

Kibabage alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika May mwaka huu nchini Gabon.

Beki huyo alijiunga na Mtibwa Sugar katika kikosi cha pili msimu uliopita na baada ya uzoefu mkubwa alioupata akiwa na Serengeti Boys, ulipelekea kuanza kukomazwa kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Mtibwa Sugar mbele ya Mratibu wa Mtibwa, Jamal Bayser

Kiongozi mmoja katika klabu hiyo alisema kuwa "ilikua furaha kwa klabu ya Mtibwa Sugar kuendelea kuwa na kipaji cha kipekee katika klabu".

“ni furaha kubwa kuendelea kuwa naye, Kibabage alikuwa katika kiwango bora tangu ajiunge nasi na ilikuwa lazima tufanye tulichokifanya na adhima yetu ni kuendelea kutunza vipaji na kuibua vipaji vipya kama Kibabage” Swabr Abubakar.

ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.

Comments

Popular posts from this blog