LACAZETTE KUIKOSA MAN UNITED JUMAMOSI HII

Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anahofia mshambuliaji Alexandre Lacazette ''hatakuwa uwanjani kwa muda'' baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu siku ya Jumatano, katika mecho ambayo walipata ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Huddersfield.

Lacazette, 26, alifunga bao la kwanza lakini alitolewa uwanjani wakati wa mapumziko na nafasi yake ikachukuliwa na Oliver Giroud.

Arsenal itaikaribisha mashetani wekundu Jumamosi katika uwanja wa nyumbani Emirates majira ya saa 20:30 usiku.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga magoli saba Arsenal tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Lyon ya Ufaransa mwezi Julai kwa kitita cha £46.5m.

''Ni bayana hatashiriki mechi ya wikendi hii,'' Wenger amesema.
''Alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wake. Atakuwa nje ya mchezo kwa muda.''

ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.

Comments

Popular posts from this blog