NJOMBE MJI YANASA WAWILI KUTOKA RWANDA

Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:

Uongozi wa Njombe Mji umesafiri hadi Rwanda kwa ajili ya kuwanasa wachezaji wawili ambao watakiongezea nguvu kikosi chao kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Njombe Mji haijafanya vizuri tangu ilipopanda ligi kuu ikiwa nafasi ya pili kutoka mwisho katika chati ya msimamo wa ligi, ikiwa na pointi nane tu baada ya kucheza michezo 11, huku ikiwa imeshinda mmoja, na imetoa sare michezo mitano na kufungwa mitano.

Njombe Mji inawaleta wachezaji hao raia wa Rwanda kwa ajili ya kuwasajili lakini lakini uongozi umegoma kuwataja majina.

Afisa Habari wa Njombe Mji, Sulvanus Mhagama alisema: "Hatuwezi kuwataja majina kwa sasa lakini wanatokea Rwanda,  tunaendelea na mazungumzo nao ili kuhakikisha tunawasajili na kuimarisha timu yetu."

"Tumeona tutoke nje ya nchi kwa sababu hapa nchini wachezaji wengi wanamikataba na klabu zao lakini hata ambao hawana mikataba wengi waowanaogombewa na klabu nyingine"alisema Mhagama.

ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.

Comments

Popular posts from this blog