OKWI KUREJEA NCHINI JUMAMOSI AU JUMAPILI

Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:

Mshambuliaji wa Simba ambaye pia ni kinara wa magoli ligi kuu Tanzania Bara anaweza kurejea nchini Jumamosi au Jumapili kuungana na wenzake.

Taarifa zinaeleza Okwi amepata nafuu kwa kiwango kizuri kabisa na anaweza kuanza mazoezi.

"Inawezekana akarejea wikindi hii, Jumamosi au Jumapili. Kama atakuwa fiti kabisa ataanza mazoezi Jumatatu," habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza.

Lakini taarifa nyingine zinaeleza, pamoja na nafuu, Okwi anaweza kuchelewa kwa kuwa mkewe alikuwa amejifungua mtoto wa pili.

"Pamoja na kuwa majeruhi, kumbuka mkewe alijifungua. Hivyo anaweza kutaka kuhakikisha mambo yamekaa vizuri katika msitari kabla ya kuondoka," kiliongeza chanzo hicho.

ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.

Comments

Popular posts from this blog