DAVID SILVA AONGEZA MKATABA MANCHESTER CITY

Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:

Kungo mshanbuliaji wa Manchester City David Silva amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ili kuendelea kuitumikia Man City hadi mwaka 2020.

Kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Man City kutoka Valencia kwa kitita cha £24m mwaka wa 2010.

Kiungo huyo ameshinda taji la ligi ya Premia mara mbili, kombe la FA na vikombe viwili vya ligi akiwa na City.

Klabu hiyo ya Pep Guardiola ipo mbele kwa pointi nane kileleni mwa ligi kuu England baada ya ushindi wa mechi 12, na ushindi ukiwa ni wa jana Jumatano dhidi ya Southamton.

Silva, ambaye amesaidia ufungaji wa magoli manane, usaidizi ambao hakuna mchezaji yeyote wa kiwango chake aliyetimiza, amesema anatarajia kuongeza tuzo zaidi Etihad.

''Najivunia kwa kile nilichojivunia nikiwa Man City kwa misimu saba na nusu sasa.

Nikiwa na Pep Guardiola Najihisi tuko katika nafasi nzuri kushinda vikombe msimu huu na kuendelea,'' alisema Silva.


''Mbinu tunayoitumia kucheza soka ni nzuri na ni furaha yangu kuwa miongoni mwao na natarajia kushinda mataji mengi miaka ijayo.

ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.

Comments

Popular posts from this blog