ZANZIBAR HEROES YASAFIRI KWA BASI ILI KUSHIRI MICHUANO YA CECAFA
Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:
KIKOSI cha Zanzibar Heroes, kimeondoka Unguja leo kwenda Kenya kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yanayotarajia kuanza December 3 mwaka huu wakitumia usafiri wa basi na boti.Msafara huo wa watu 34, wachezaji 24 na viongozi 10, wamendoka majira ya saa 9:00 asubuhi na boti ya Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam, walipofika Dar es Salaam, walipanda basi kwenda Kenya, kwa kutumia njia ya Tanga.
“Tumaini la safari yetu hii itakuwa yenye mafanikio makubwa kwa Zanzibar nzima, kikubwa tunaomba dua zenu tusafiri salama kwenda na kurudi,” alisema Kocha wa timu hiyo Hemed Suleiman ‘Morocco’.
Miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Ahmed Ali ‘Salula’, NassorMrisho, Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’,Abdallah Haji ‘Ninja’, Mohd Othman Mmanga, Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ , Adeyum Saleh ‘Machupa’, Haji Mwinyi Ngwali, Issa Haidar ‘Mwalala’, Abdulla Kheir ‘Sebo’, pamojana Ibrahim Abdallah .wengine ni Abdul-swamad Kassim, Abdul Aziz Makame, Mudathir Yahya, Mohammed Issa ‘Banka’, Amour Suleiman ‘Pwina’, Hamad Mshamata,Suleiman Kassim ‘Seleembe’, Kassim Suleiman , Feisal Salum , Khamis Mussa ‘Rais’, Mwalimu Mohd, Seif Abdallah ‘Karihe’ na Ibrahim Hamad Hilika.Awali wachezaji hao walikuwa 30 na kulazimika kuachwa 6 ambao wengine waliachwa kwasababu ya majeruhi akiwemo Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ) na Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege) huku wengine walioachwa ni Mbarouk Marshed (Super Falcon) na Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi).
Hata hivyo kwa upande wa viongozi ambao wanaungana na wachezaji hao katika msafarawa kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya mashindani ya Chaleng na Hemed Sulaman Morocco Kocha Mkuu, Ali Sulaiman Kocha Msaidizi, Khamis Haji Mkuu wa msafara, Abdul Wahab Dau Meneja wa timu, Mohamed Yussuf Daktar wa timu, Hafidh Muhidini Msaidizi wa shughuli za timu pamoja na Abubakar Khatib Mwandishi wa Habari.
ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.
Comments
Post a Comment