AZAM KUONESHA MUBASHARA MICHUANO YA CECAFA 2017
Usipitwe na Habari zote za Michezo, Usajili,na Magazeti, Install Bure App Yako ya Kijanja ya Nijuzehabari Hapa chini:
KAMPUNI ya Azam Media imethibitisha kuonyesha moja kwa moja mashindano ya soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Chalenji) yatakayoanza nchini Kenya, Disemba 3.Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alisema kampuni yake imeamua kujitosa kuonyesha mashindano hayo ili kuunga mkono harakati za kuinua mchezo wa soka kwa ukanda huu.
"Tumekuwa na majadiliano na Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hatimaye tumefanikiwa kupata haki za kuonyesha mashindano haya ambayo yana historia kubwa barani Afrika,”alisema Mhando.
“Kikubwa tumejiandaa kikamilifu kuwapa wapenzi wa mpira wa miguu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo timu zetu zitapiga kambi nchini Kenya katika miji ya Machakos na Kakamega, tukiwa na vifaa vya kisasa zaidi ambavyo vitafanya twende katika hatua za juu zaidi katika matangazo ya mpira wa miguu." Alifafanua.
Jumla ya timu tisa zilizopangwa katika makundi mawili zitashiriki mashindano hayo ambapo kundi A lina timu za Libya, Tanzania Bara, Kenya, Zanzibar na Rwanda wakati kundiB litakuwa na nchi za Burundi, Uganda, Ethiopia na Sudani Kusini
ILI KUZIPATA HABARI ZETU KWA HARAKA ZAIDI USIKOSE KULIKE PAGE YETU HAPA CHINI BOFYA LIKE.
Comments
Post a Comment