TFF YAWEKA WAZI VIINGILIO, TAIFA STARS VS BOTSWANA, 02-09-2017.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Botswana utakaofanyika Jumamosi Septemba 2, mwaka huu. Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) viingilio vitakuwa Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko. Wakati huo huo, Kiungo Taifa Stars, Simon Msuva tayari amejiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco baada ya Shirikisho la Soka Morocco na timu yake kumfanyia mpango wa visa ya muda mrefu iliyomwezesha kusafiri. Mchezaji ambaye imeshindikana kuja ni Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno. Sababu ni taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa. Nyota wengine walikwisha kuripoti ni pamoja na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi B...