USAJILI: RASMI CHAMBERLAIN ATUA LIVERPOOL.
Klabu ya Liverpool imefanikiwa Kumsajili Winga mwenye kasi Alex Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal kwa ada ya Pauni Milioni 35.
Chamberlain amesajiliwa Liverpool ikiwa ni baada ya yeye kukataa kujiunga na Chelsea ambao walifika dau kwa ajili ya kumsaini, lakini hakuwa tayari kutua Darajani hapo, akitoa sababu kuwa Chelsea walitaka kumfanya beki kitu ambacho yeye hakitaki, huku akiwa anataka kutumika kama Kiungo wa kati.
Like Page yetu hapa chini ili uwe wa kwanza kupata habari zetu zote za Michezo na Usajili
Comments
Post a Comment