OKWI KAMA JUMA NATURE, AMERUDI NA 'MAKEKE YAKE YA LONGI'
Makala hii ilitoka kwenye gazeti la Mwanaspoti la Jumatatu ya Agosti 21. Kwa heshima yake ya leo dhidi ya Misri na ile dhidi ya Ruvu Shooting, naomba kuirudia hapa!
Kwenye wimbo wa NAJA wa Squeezer akimshirikisha Juma Nature, kuna mstari Nature anasema 'na ndo nsharudi na makeke yangu ya longi'
Wimbo huu ulitoka mwaka 2007 katika kipindi ambacho nyota ya Juma Nature ilionekana kama inaanza kufifia baada ya kung'aa kupita kawaida mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kwa hiyo hapa Nature alitaka kutoa ujumbe kwa watu waliokuwa na hofu kwamba Nature 'ndo basi tena'...akawambia anarudi na 'makeke yake ya longi'.
Kwa waliomsikia Nature kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, watakuwa wanayajua makeke yake. Kuanzia kwenye collabo na Mabaga Fresh ya "Mtulize", njoo kwenye "Mtani Jirani" na Joint Mob, sikiliza "Umuhimu" na Lady Jaydee, au "Ndiyo Mzee" aliyofanya na Prof. Jay. Hapo hujagusa kazi zake mwenyewe kama "Jinsi Kijana", "Hili Game", Kighetogheto" nk. Bila kusahau alizoimba na wanaye wachuja nafaka kama "Ya Leo Kali", "Mzee Wa Busara" nk.
Humu mote Nature alifanya makeke ya ajabu. Mtiririko wake wa mashairi na maneno yake ya uswahilini ni vitu ambavyo vilimpambanua Nature kama kijana mwenye kipaji cha hali ya juu.
Lakini kuanzia katikati ya miaka ya 2000, ni kama makeke yake yalianza kupotea na ndipo akaja na ujumbe huu "ndo nsharudi tena na makeke yangu ya longi".
Kwenye wimbo huo ambao Nature aliikipamba vilivyo kiitikio na kuimba verse ya kwanza, kabla ya kufikia hapo kwenye makeke yake ya longi, Nature aliongea lugha anazozijua mwenyewe katika yale makeke yake, "Mwagia asidi majivu yenye mkaa wenye kufuka manjano, volcano, mpiga veno ingieno alenieno, mapigamieno".
Haya ndiyo makeke ambayo mashabiki wa Nature waliyazoea tangu wamfahamu...long time(longi). Anachanganya changanya maneno mpaka anamvuruga msijilizaji.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmamuel Arnold Okwi amejerea Simba SC kwa mara ya tatu na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza na pekee kuhama na kurudi Simba katika viwili vitatu tofauti, kwa lugha ya kimpira tunaita hat-trick. Okwi anaungana na Abdallah Kibaden kuwa wachezaji pekee wa Simba waliopiga hat trick za kihistoria. Kibaden alipiga hat trick kwenye mchezo wa Simba na Yanga mwaka 1977 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza na pekee mpaka sasa kufunga mabao matatu kwenye mchezo wa watani hao wa Kariakoo.
Yes Okwi amerudi...ni kweli Okwi amerudi na kwa anavyoonekana, amerudi kama Juma Nature kwenye NAJA, 'na makeke yake ya longi'
Emmanuel Okwi anarudi Simba akitokea klabu yake ya utotoni, SC Villa Jogoo ya Uganda ambapo hapo pia amepiga hat trick ya kuhama na kurudi. Aliondoka klabuni hapo 2009 kujiunga Simba, akarudi tena 2014 akitokea Etoile Du Sahel na Februari mwaka huu akarudi tena akitokea SønderjyskE ya Denmark.
Wakati akimtambulisha Okwi kwa waandishi wa habari, Rais wa klabu hiyo, Ben Immanuel Misagga, alisema, "tumemsajili Okwi kwa sababu tunataka mabao."
Halafu akamgeukia Okwi mwenyewe baada ya kumkabidhi jezi namba 7, akamwambia, "na kwako wewe (Okwi), tunataka mabao na ni matarajio yetu utatufungia bao moja angalau kila mechi.”
Okwi alijiunga Villa kipindi cha dirisha dogo la usajili na katika nusu msimu wake alioitumikia klabu hiyo, alifunga mabao 10 katika mechi 12. Bila shaka aliitikia wito wa Rais wa klabu.
Huu ni wastani mzuri zaidi kwa Emmanuel Okwi kwani katika hat trick zake za nenda rudi Simba na Villa, ni misimu michache sana yenye kumpatia tarakatibu za uwiano huu wa idadi ya mechi na mabao ya kufunga.
Alipokuwa Simba, msimu wake bora kabisa ulikuwa ule wa 2011/12 alipofunga mabao 12 msimu mzima katika michezo 20 akihitimisha na mabao 2 Mei 6, 2012 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya mahasimu wao wakuu, Yanga.
ALIVYOJIUNGA SIMBA
Mwaka 2009, makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' alikwenda Kampala Uganda kuangalia namna ya kumsajili mshambuliaji tishio wa SC Villa, Brian Umony. Lakini kwa bahati mbaya mchezaji huyo alikuwa na mipango yake mingine, alipata dili la kwenda Super Sport United ya Afrika Kusini. Baada ya kukwama kwa Umony, Kaburu akapata taarifa kwamba kuna 'wonder kid' anaitwa Emmanuel Arnold Okwi aliyekuwa amepandishwa mwaka huo huo kutoka timu ya vijana. Kaburu akafanya mipango na kumsainisha.
Okwi akatua Simba na kutengeneza safu kali ya ushambuliaji na akina Mussa Hassan ‘Mgosi’, Uhuru Selemani, Ulimboka Mwakingwe na Mohamed Kijuso wakisambaziwa huduma na Haruna Moshi Boban.
Wachezaji wenzake wa kigeni kama beki Joseph Owino kutoka Uganda na kiungo Hillaly Echessa kutoka Kenya waliifanya Simba iwe tishio katika msimu huu ambao mnyama alichukuwa ubingwa bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Japo Mussa Hassan Mgosi ndiye aliyekuwa staa wa Simba na kinara wa mabao akifunga mabao 18 yaliyomfanya kuwa mfungaji bora wa VPL 2010, Okwi aliendelea kupevuka na kujiimarisha kidogo kidogo na kuwa hatari.
Taratibu akajenga heshima na jina kwa kocha mpya Profesa Milovan Curkovic aliyechukua nafasi ya Mzambia Patrick Phiri. Lakini kitu kipekee kilichobaki kwa mashabiki wa Simba, kilikuwa kitendo chake cha kutowafunga Yanga.
Kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2011/12, Okwi alipoteza nafasi kadhaa halafu mwisho wa mchezo Simba wakafungwa 1-0 kwa Yanga kwa bao la mzambia Davies Mwape.
Hapo mashabiki waliumia sana na kumuona Okwi kama mchezaji wa mechi ndogo kwa sababu kwa mashabiki wa hizi timu za Kariakoo, hakuna mechi kubwa kama ya wao kwa wao. Mchezaji atakayefanya vizuri kwenye mechi hii basi huyo ni mchezaji wa mechi kubwa. Mashabiki wengi wa Simba walikuwa bado na kumbukumbu ya mshambuliaji wao hatari, Zamoyoni Mogela ambaye licha ya kuvaa jezi nyekundu kwa zaidi ya miaka 10, aliifunga Yanga mara moja tu! Hawakutaka hili litokee kwa Okwi na mwaka 2012 wakati Simba wakirudi nyumbani kutoka Tunisia walikowaondosha mashindanoni E.S Setif huku Okwi akifunga bao la hatari, mashabiki waliipokea timu kwa shangwe kubwa wakiwa na mabango yenye ujumbe kwa Okwi "Okwi tunashukiru sana kwa mchango wako, lakini mbona huifungi Yanga"?
Jibu la Okwi mara zote lilikuwa moja tu, "muda ukifika nitawafunga tu".
Naam, muda ukafika Mei 6, 2012 na Okwi akawafurahisha mashabiki wake. Akafunga mabao 2 na kusababisha penati 3 katika mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah ambaye ni 'Yanga lia lia' na katika kudhihirisha hilo, hivi sasa ni mjumbe wa kuchaguliwa wa kamati ya utendaji ya Yanga.
Katika mchezo huu ulioisha kwa ushindi wa 5 - 0, mashabiki wa Simba waliridhika kwamba kweli Okwi ni mchezaji wa mechi kubwa.
Machi 8, 2015, Okwi akaifunga tena Yanga kwa 'bao la akili nyingi' akimshinda mbio Mbuyu Twitte na kumzidi maarifa kipa Ally Mustapha Barthez. Mashabiki wa Simba wakambatiza jina la 'jua kali kiboko cha nguo mbichi'.
Safari zake za Tunisia na Denmark, zimempevusha zaidi kuliko kummaliza kama wengi wanavyodhani.
Aliporudi Simba msimu huu, mechi yake ya kwanza hapa nyumbani ilikuwa kwenye tamasha la Simba Day dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda, akatoa pasi ya bao. Mechi ya pili ikawa dhidi ya Mtibwa Sugar, akafunga bao moja.
Huu ni wastani mzuri sana kwa mshambuliaji na hii inadhihirisha kwamba Emmanuel Arnold Okwi bado anayo makeke yake ya longi.
Na Zaka Zakazi
Like Page yetu hapa chini ili uwe wa kwanza kupata habari zetu zote za Michezo na Usajili
Kama una picha,Video au Habari zinazohusu Michezo tutumie WhatsApp namba +255756658100.
Sambaza habari hii Facebook, Sambaza Twitter, Sambaza WhatsApp Mshirikishe mwenzako

Comments
Post a Comment