SIMBA SC: TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA MAJERUHI 31-08-2017.

Daktari amuongezea wiki mbili Shomary Kapombe, ni baada ya kutoridhishwa na maedeleo yake.

Huku mashabiki wa Simba wakiwa wana hamu kubwa ya kumuona uwanjani, daktari amemuongezea wiki mbili nyingine za matibabu beki Shomari Kapombe.

Kapombe alitarajia kurejea mazoezini wiki hii, lakini daktari ametaka uhakika wa mambo na kumuongezea wiki mbili ili awe vizuri zaidi.

"Hataanza mazoezi, ana wiki mbili nyingine. Daktari anataka kuona tatizo lake la nyonga linaisha kabisa," alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

Kuhusu Haruna Niyonzima Ndugu Msomaji wa Nijuzehabari Blog, Niyonzima ameanza mazoezi, pamoja na John Bocco kwa pamoja wameanza mazoezi hapo jana.

Like Page yetu hapa chini ili uwe wa kwanza kupata habari zetu zote za Michezo na Usajili
Kama una picha,Video au Habari zinazohusu Michezo tutumie WhatsApp namba +255756658100. Sambaza habari hii Facebook, Sambaza Twitter, Sambaza WhatsApp Mshirikishe mwenzako

Comments

Popular posts from this blog