Posts

Showing posts from May, 2019

Orodha kamili ya washindi wa MO Simba Awards 2019

Image
Usiku wa kuamkia leo kulitolewa tuzo za Mo Simba Awards 2019 katika hoteli ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam. Chini ni majina ya washindi. 1. Aishi Manula ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka. 2. Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka. 3. ames Kotei ameshinda Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka. 4. John Bocco ameshinda Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka. 5. Rashid Juma ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka. 6. Mwanahamisi Omary Shurua ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka. 7. Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Wachezaji. 8. Meddie Kagere ameshinda Tuzo ya Mfungaji Bora wa Mwaka. 9. Tuzo ya Heshima imekwenda kwa Azim Dewji. 10. Goli la Clatous Chama dhidi ya Nkana limeshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka. 11. Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Mo Simba 20 from MUUNGWANA BLOG

MAGAZETI YA LEO 31/5/2019

Image
from MUUNGWANA BLOG

Jinsi yakumfanya akukubali mapema

Image
Yawezekana kuna mtu hisia zako ndipo zinapoamkia, naamisha unampenda kweli mpaka inafika mahali huelewi kinachondelea, njia nzuri na rahisi zitakazomfanya mtu huyo aweze kukubali mapema mara baada ya kumuonesha hisia zako ni pamoja na kufanya mambo yafutayo: Uwe na muonekano mzuri Wanawake wanapenda wanaume wasafi na watanashati kwa hiyo ukiwa msafi na mtanashati utakua na mvuto kwake. Hivyo utakapoamua kumshawishi kufanya mapenzi itakua rahisi yeye kuwa rahisi kukubali. Mfanye ajisikie huru Ni rahisi mwanamke kufanya mapenzi na mtu anayejisikia huru mbaele zake na ambaye yupo huru kuongea na kufanya nae mambo mengine ya kawaida katika maisha. Kwa hiyo ili uweze kumshawishi mwanamke kufanya mapenzi na wewe njia nzuri ni kumfanya ajisikie yupo huru mbele yako na kasha atakua huru kufanya mapenzi na wewe. Mfurahishe Mfanye ajisikie mwenye furaha kila anapokuwa na wewe na atamani kuwa na wewe. Akishajiskia mwenye furaha kila anapokuwa na wewe ni rahisi kushawishika kuwa na wewe...

VIDEO: Kagere, Nyoni watamba tuzo za Mo Dewji/ Okwi, Niyonzima na Salamba wabaki hoi

Image
Hatimaye tuzo za MoSimbaAwards ambazo zilianzishwa na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Mohammed Dewji "Mo Dewji" kuanzia mwaka jana, zimetolewa tena leo katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Regency zamani ikifahamika kama Kilimanjaro Hotel iliyopo jijini Dar es Salaam. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE from MUUNGWANA BLOG

Mbinu za kuwa bora katika maisha yako

Image
Katika maisha yako unahitaji kutambua mambo mbalimbali yatakayokufanya uweze kuwa bora zaidi, huwezi kusema unataka mafanikio wakati mambo ambayo unajua ni yale mwaka 47. Hivyo kwa kila jambo ambalo unataka kuwa bora katika eneo hilo ni vyema ukajua ni kwa namna gani utaweza kuwa bora. Swali linaweza kunijia ghafla, sasa nafanyaje ili kuwa bora? Ipo hivi ukitaka kuwa bora katika maisha yako unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;  Kuwa mwaminifu.  Bila uaminifu katika maisha yako, basi ujue fika mafanikio utayasikia kwa majirani zako waliofanikiwa. Na moja kati ya sabau za kushindwa kufanikiwa katika maisha yetu husasani sisi vijana ni kwamba wengi wetu hatuaminiki. Wapo baadhi ya watu wakipata kazi huwa wanakuwa wanyenyekevu sana, ila baada siku chache  mara baada ya kuizoea kazi hiyo huwa wanakuwa ni watu ambao hawaminiki hata chembe, roho na hulka zao ni kutaka kufanikiwa kwa haraka, wapo baadhi ya watu hudiriki hata kumuibia mtu ambaye ameawajiri. Kufanya hivyo huf...

Fahamu kuhusu ugonjwa wa kipindupindu kiundani zaidi

Image
Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika. Nchini Tanzania hususani katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, haishangazi basi kusikia kila mwaka kuna mlipuko wa ugonjwa huu pamoja na juhudi kubwa za serikali na mamlaka zake kujitahidi kuhimiza wananchi kupambana na ugonjwa huu. Kwanini nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na ugonjwa huu? Moja wapo ya changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ni jamii kutokuwa na uhakika wa kupata Maji safi na salama, pamoja na kutokuwa na mazingira safi kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na mlipuko wa kipundupindu au huwa katika hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo. Kipindupindu hus...

Jinsi ya kupika futari ya Vibibi vya Tui la Nazi

Image
Vipimo Mchele 2 Vikombe 1. Tui la nazi zito 2 Vikombe 2. Hamira 1 Kijiko Cha chai 3. Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu 4. Iliki Kiasi upendavyo 5. Sukari Kiasi upendavyo 6. Yai 1. Vipimo vya Tui la Kupaka 1. Tui la nazi 2 Vikombe 2. Hiliki ya unga Kiasi upendacho 3. Sukari Kiasi upendacho 4. Unga wa ngano 1 Kijiko cha supu. Namna ya Kutayarisha na Kupika • Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo. • Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito. • Osha na loweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi. • Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini. • Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya. • Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure/uvimbe Ukishafura, weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo) Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote. Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au saml...

Fahamu matumizi ya viatu mbalimbali kwa wanawake

Image
Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na  mavazi yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu  na wapi hasa na vipi vikitumika vinapendeza zaidi. 1.Viatu vya ngozi vya kufunika Viatu vya kufunika vipo virefu sana, vyenye urefu wa wastani na vifupi kabisa. Mara nyingine haviwi vya ngozi kabisa bali ni kama vina plastiki na pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele.Viatu virefu zaidi mara hupendeza zaidi kuvaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na kupunguza ufanisi. Viatu vyenye urefu wa wastani unaweza kuvaa popote iwe kazini, kanisani, kwenye sherehe n.k. Viatu vya chini kabisa vinakuwa vyenye matumizi zaidi wakati unamatembezi mengi. Havifai sana kuvaa kwenye sherehe za usiku hasa kama unavaa nguo maalumu ya usiku. Vinafaa sana kwa...

Mwanafunzi darasa la nne akutwa na mimba ya miezi saba

Image
Mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Welezo halmashauri ya Shinyanga mwenye umri wa miaka 11 amekatisha masomo baada ya kupimwa na kukutwa na ujauzito wa miezi saba. Akizungumza katika  kikao cha wenyeviti wa vitongoji 30 vya kata ya Usanda pamoja na wazee wa kimila, ofisa ustawi wa jamii wa halmashauri hiyo, Elizabeth Mweyo amesema mwanafunzi huyo alipewa ujauzito mwaka 2018  na mwanaume ambaye hajafahamika. Amesema aliendelea na masomo kama kawaida na baadaye mwalimu wake alimgundua  na baada ya kupimwa alibainika kuwa na ujauzito. “Tumekutana hapa lengo kubwa ni kujadili na kupanga mikakati ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni tatizo bado ni kubwa, watoto wanakatisha ndoto zao kama tukio la mwanafunzi wa darasa la nne kukatisha masomo yake,” amesema Mweyo. Amesema kuanzia Januari hadi Machi, 2019 wanafunzi 26 wamepata ujauzito na watatu kati ya hao ni wa Shule za Msingi, kuwataka wenyeviti wa vitongoji kuunganisha nguvu kukabiliana na tatizo hilo. ...

CWT wafunguka kuhusu tuhuma za Ufisadi zilizoandikwa kwenye gazeti la Jamuhuri

Image
Na.Enock Magali,Dodoma Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa ufafanuzi juu ya kile kilicho andikwa katika gazeti la JAMUHURI la tarehe 28 ya mwezi May,katika  ukurasa wake wa  mbele,iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho  Ufisadi ,Upendeleo  Chama cha walimu. Akizungumza na vyombo vya habari jijini dodoma, Rais wa Chama hicho Leah Ulaya,amesema kuwa  taarifa iliyochapishwa  kwenye gazeti hilo,haziendani  na  uhalisia  wa kile kinacho fanyika ndani  ya chama hicho  kwa sasa. "Tunafata taratibu,kanuni na sheria zetu kulingana na katiba yetu ya CWT na chama chetu kitaendelea kuwa rafiki wa waandishi wa habari na vyombo vya habari vinavyozingatia misingi,weledi na taaluma ya habari,na tunategemea sana ushirikiano wenu katika kufikisha ujumbe kwa kadri tutakavyo wahitaji," Alisema. Aidha, ameongeza kuwa habari hiyo kwa namna moja ama nyingine, ilikuwa na lengo la kuwafedhehesha, na pia  kukichafua chama hicho, pamoja na...

Nafasi za kazi Leo Mei 30

Image
Job Opportunity at Letshego Bank, Chief Operations Officer (COO) Job Opportunity at UNDP Tanzania, National Project Coordinator Job Opportunity One Acre Fund Tanzania, Deputy Field Training Supervisor Job Opportunity at BRAC Tanzania, Financial Analyst Job Opportunity at CVPeople Africa, Leadership And Community Engagement Intern 2 Job Opportunities at CVPeople Africa, Finance And Administration Interns from MUUNGWANA BLOG

DC aagiza kila Mwananchi kudhibiti mimba kwa Wanafunzi

Image
Na Amiri kilagalila-Njombe Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Ally Kasinge ameagiza kila mwananchi kuhakikisha anashirikiana na serikali kudhibiti mimba kwa wanafunzi katika wilaya hiyo kutokana na takwimu ya wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni kuendelea kuongezeka. Kasinge ametoa agizo hilo katika kikao cha cha tathmini ya elimu kilichofanyika wilayani hapo mara baada ya kusomewa takwimu za idara ya elimu zilizobainisha wanafunzi 22 kukatishwa masomo mwaka jana huku kuanzia januari 2019 hadi sasa wanafunzi 6 wakikatishwa masomo yao. "Uwe kiongozi,uwe mwananchi,uwe mchungaji,uwe mwalimu,uwe askari lazima tuhakikishe tunafanya kazi ya kudhibiti mimba ya wanafunzi wa kike katika wilaya yetu, kila mtu mtu atimize wajibu wake na kwenye hili hatutamuacha mtu endapo haya yakiendelea,takwimu hizi mmeziona"alisema  Kasinge Kwa mujibu wa takwimu za idara ya elimu Zilizotolewa na Maofisa elimu sekondari na Msingi Akiwemo Loice Mgonja na Fredrick Mhanze wilaya...

Utabiri wa Hali ya Hewa wa siku tano na athari zinazoweza kutokea

Image
from MUUNGWANA BLOG

Watanzania 100,000 walinda amani nchi za Afrika

Image
Idadi ya Watanzania wanaofanya shughuli za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali imefikia 100,000 huku 3800 wakiwa wamepoteza maisha tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa kutoa walinzi mwaka 1948. Hayo yalisemwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi jijini Dare s Salaam katika siku ya kuwakumbuka na kuwapongeza walinzi wa amani katika nchi mbalimbali. "Idadi walinda amani karibu 100,000 sasa hivi wako katika nchi mbalimbali za Afrika, hivyo tunawapongeza kwa kazi nzito waliyonayo lakini pia kuwakumbuka walinzi 3,800 waliopoteza maisha kuanzia mwaka 1948 tangu ilipoanza kazi ya ulinzi wa amani,"alisema Dk Mwinyi. Dk Mwinyi alisema Tanzania ina jukumu la kulinda amani, ndio maana inawajibika kuwapeleka walinzi katika nchi mbalimbali ili kuwalinda raia wasiokuwa na hatia wanaotaabika na kukosa amani katika nchi zao. Alizitaja baadhi ya nchi ambazo kwa sasa Tanzania imepeleka walinzi wa amani kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Afri...

Wakenya washangazwa na Vazi la Waziri Mkuu wa Fiji

Image
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonyesha kupigwa na butwaa na vazi alilovaa Waziri mkuu wa Fiji Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi. Waziri mkuu Bainimarama ambaye ni mwanamume alikuwa amevalia suti ya sketi na viatu vya wazi (sandozi) wakati alipopata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa makazi nafuu katika eneo la Ngara jijini Nairobi. Vazi alilovalia ni maarufu nchini Fiji kwa wanaume wa likifahamika kama na jina Suti ya Sulu. Suti ya Sulu inachukuliwa kama vazi la kitaifa la Fiji na huangaliwa kama utambulisho wa jamii ya Wafiji . Vazi hili ambalo huwa wakati mwingine sketi yake inakatwa katwa upande wa chinihuvaliwa na wanaume na wanawake wa Fiji. Lakini Sulu ya wanawake hufahamika kama Sulu-i-ra, Urefu wa vazi hili unategemea na mtu apendavyo kuanzia chini ya magoti au urefu wa kufika kwenye kisigino. Zamani ulikuwa unavaliwa mkanda tumboni. Hata hivyo wanaume wa kisasa wanaweza kutumia pini. ...

Jibu la Serikali kwa waliojenga nyumba bondeni

Image
Bunge limeelezwa kuwa serikali hairuhusu na haitavunja makazi ya watu waliojenga maeneo hatarishi ikiwamo mabondeni. Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalumu,  Zainab Amiri (CUF). Katika swali lake, mbunge huyo alisema kuna baadhi ya watu wanajenga kwenye mabonde, wengine jirani na hifadhi ya barabara na reli lakini serikali hukusanya kodi za maeneo na majengo katika maeneo hayo. “Je, serikali inaeleza nini kuhusu kadhia hii, ili mwananchi ajenge mahali husika lazima apate kibali, je, nini adhabu ambayo wanapewa wanaotoa vibali kwenye maeneo hatarishi,” alihoji. Akijibu swali hilo, Waziri Lukuvi amesema utoaji wa leseni za makazi hautafanyika kwa watu waliojenga maeneo hatarishi. “Ni kweli kuna watu wanajenga kwenye hifadhi za barabara na hifadhi za miundombinu mingine na mabondeni lakini wamefanya hivyo kinyume na sheria, serikali hairuhusu na hata zo...

Ashikiliwa na TAKUKURU kwa kumpa rushwa Mwanasheria wa CCM

Image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia watu watatu akiwamo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa ambaye anatuhumiwa kutoa rushwa ya Sh 200,000 kwa Wakili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Goodlucky Mwangomango, ili ampe upendeleo kwenye kikao cha kujadili mikataba ya miradi ya chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema, tukio hilo limetokea Mei 29, mwaka huu, saa nne asubuhi, maeneo ya Sea View Upanga kwenye mgahawa wa Central Park. Amesema Chandulal ambaye ni mpangaji wa  maeneo ya biashara ya CCM alitoa kiasi hicho ili apewe upendeleo kwenye kikao cha chama hicho cha kufanya marejeo ya mikataba. “Mtuhumiwa Chandulal atafikishwa mahakamani chini ya kifungu Cha 15 (1), (b) cha Sheria ya Takukuru Na.11/2007,” amesema Myava. Myava alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili. from MUUNGWANA BLOG

Wanaoiga nembo kusakwa

Image
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, amekitaka Kiwanda cha kuunganisha magari cha Rajinder kuwasilisha malalamiko ya baadhi ya watu kuiga teknolojia yao kwa maandishi kwa Tume ya Ushindani nchini (FCC). Alisema waigaji hao wanaodaiwa kughushi na kutumia nembo ya Rajender,  taarifa zao zikifikishwa kwa maandishi watashughulikiwa kwa wakati. Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda hicho na kuwataka waandike barua rasmi  ili serikali iweze kushughulikia malalamiko hayo na hatua kali za kisheria zichukuliwe. “Naiagiza tume ya usimamizi kuhakikisha inafika katika kiwanda cha Rajender na kushughulikia malalamiko hayo, ili kutokomeza na kudhibiti watu wasio waaminifu wanaotumia nembo ya Rajinder,” alisema na kuongeza kuwa “Hatutamvumilia mtu yeyote atakayemsababishia mwekezaji hasara ya  kufunga kiwanda chake kwa ajili ya watu ambao si waaminifu wanaonakili na kukopi nembo ya mtu anayelipa staiki zote za serikali…”alisema. Aliahidi kuwa serikali it...